Header Ads

ad

Breaking News

Cheka ajivunia kutajirisha mabondia wenzake


Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka, amesema anajivunia kubadilisha malipo ya mabondia katika mapambano kutokana na kiwango chake kizuri katika masumbwi.
 Cheka amesema, amesaidi kubadili hali ya malipo kwani hivi sasa wanalipwa mamilioni ya fedha kwa pambano moja watakalopigana naye.

Amesema awali mabondia walikuwa wakilipwa fedha kidogo, lakini tangu aanze kuwatangwa mabondia katika uzito tofauti, hupanda ulingoni kwa gharama kubwa, hivyo huwasaidia mabondia wenzake.

Amesema kutokana na hali hiyo, imewafanya mabondia wengi kutaka kupigana naye na kuongeza kuwa, uwezo wake unachangia kuwapa sifa mabondia wengine.

Bondia huyo amesema kuwa, alianza mazoezi madogo madogo kwa kujiandaa na pambano la kufunga mwaka dhidi ya Kalama Nyilawila,  linakalofanyika Desemba 31, mwaka huu katika Uwanja wa Jamuhuri, Morogoro.

No comments