Mtanga yahitaji milioni 150 kuunga mkono juhudi za Rais Samia
Msafiri Mtanga akionesha moja ya mashine ya kukanda ngano
Na Omary Mngindo, Kibaha
KAMPUNI ya Mtanga Polymachinery ya Kibaha Mkoa wa Pwani inahitaji Shilingi milioni 150, ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu za kuhamasisha matumizi ya nishati safi.Kampuni hiyo inayojihusisha na utengenezaji wa majiko banifu sanjali na yanayotumia umeme tayari imeshayauza majiko katika Kampuni na taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi zikiwemo shule.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Msaidizi Msafiri Mtanga, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Kibaha Picha ya Ndege ambapo pia inajihusisha na uuzaji wa makaa ya mawe.
"Kampuni yangu mbali ya kutengeneza majiko hayo banifu pia tunauza makaa ya mawe, ambapo tunauza kuanzia kilo moja ambayo inaweza kupika hata maharage ambapo mtumiaji anatumia nusu na usiishe," alisema Mkurugenzi huyo.
Ameongeza kuwa, kutokana na kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu za kuhamasisha matumizi hayo, Kampuni hiyo inatafua kiasi cha Shilingi milioni 150 ili iendelee kuunga mkono juhudi hizo kwa kuuza majiko na makaa hayo katika taasisi.
"Katika kuendelea huko kuunga mkono juhudi hizo pia tunawashauru waTanzania kurejesha utengenezaji wa vyugu kwani vinafaa sana katika matumizi ya makaa hayo, kwani makaa yana moto mkali ambapo kwa vyungu vitaokoa fedha nyingi kwa watumishi," alisema Mkurugenzi huyo.
"Katika kupambana na hilo pia tunatengeneza majiko kwa ajili ya familia sanjali na sufuria zake, unanua makaa ya mawe yana moto mkali hivyo kuna sufuria zake Maalumu ambazo sisi tunazitengeneza," alisema Mtanga.
Alimalizia kwa kusema kuwa kampuni hiyo pia inatengeneza mafuta ya nazi, na ipo katika mpango wa kuzalisha maji safi na salama sanjali na mota zinazozalisha umeme, kwa wanaoishi pembezoni ambapo hakujafikiwa na miundombinu hiyo ambao wanaweza kutoa oda wakatengenezewa.
No comments