Header Ads

ad

Breaking News

Kamati ya Amani Chalinze yaandaa kongamano la amani

Kiongozi wa Kamati  Amani Jimbo la Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Alhaj Hamis Nassor 

Na Omary Mngindo, Chalinze

KAMATI ya Amani Jimbo la Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, limeandaa kongamano kubwa la kuiombea nchi kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu. 

Kiongozi kamati hiyo Alhaj Hamis Nassor amesema kuwa Kongamano hilo litafanyika Oktoba 4 kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 8 mchana. 

Amesema kuwa, kongamano hilo litahusisha viongozi wa serikali, dini zote na wananchi litafanyika kwenye viwanja vya Polisi vilivyopo Bwilingu Chalinze mjini.

 "Kamati yetu ya Amani Jimbo la Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, tumeandaa kongamano hilo kwa lengo la kuzungumzia uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Oktoba mwaka huu," amesema Alhaj Nassor. 

Ameongeza kuwa, "Kongamano hilo litahusisha viongozi wa serikali, dini na vijana wote wa Chalinze kwani lengo kuu ni kuwahamasisha waTanzania waishio Chalinze na vitongoji vyake katika kuelekea uchaguzi Mkuu," amesema Alhaj huyo.

Alisema kwamba viongozi wa dini nchini wanajukumu kubwa la kuhamasisha amani, upendo na mshikamano ili nchi iendelee kuwa kisiwa cha amani. 

"Watanzania tuna kila sababu ya kujivunia amani tuliyonayo kwani mataifa mengi yanaitamani, lakini wanashindwa, hivyo tusiichezee," amemalizia Alhaj huyo.

No comments