Achahofu awatoa hofu wanaSimba
Na Omary Mngindo, Mlandizi
WANACHAMA, wapenzi, mashabiki na wakereketwa wa Klabu ya Simba wametakiwa kutokuwa na hofu wakati huu wa usajili, na kuachana na mitandao inayosambazwa kuhusiana na zoezi la usajili.
Hofu hiyo imeondolewa na Katibu wa tawi la Simba Nguvu Moja lililopo Mlandizi Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Eli Achahofu, akizungumza na Waandishi mjini hapa ambapo amewataka wanaSimba kutulia katika kipindi hiki.
Alisema kuwa wakati huu wa vuguvugu la usajili wa wachezaji kuelekea Ligi Kuu ya msimu ujao, kunakuwaga na mambo mengi yanayotokea kwenye zoezi hilo, huku akieleza kwamba uongozi wa klabu umemkabidhi jukumu la kusimamia usajili benchi la ufundi chini ya kocha Mkuu kocha Fadlu Davis.
"Kwanza naupongeza uongozi wa klabu yetu chini ya Mfadhili Mkuu Mohamed Dewj MO, kwa uamuzi mzuri wa kumkabidhi kocha Fadlu jukumu la kusajili wachezaji, nina imani kubwa kwamba msimu ujao tutakuwa na timu nzuri yenye ushindani," alisema Achahofu.
No comments