Header Ads

ad

Breaking News

Wanachama wa UWT Bagamoyo watakiwa kufanya kampenzi za kistaarabu

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Wilaya ya Bagamoyo, Mariamu Mkali, akizungumza na wajumbe wa braraza hilo

Na Omary Mngindo, Msata

WANACHAMA wa Umoja wa Wanawake  (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wametakiwa kwenda kufanya kampeni za kistaarabu.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Umoja huo, Mariamu Mkali, katika Baraza la kawaida lililofanyika katika Kata ya Msata, Halmashauri ya Chalinze wilayani hapa, amesema wakati ukifika wayazingatie hayo.

Mkali amesema kuwa wote ni wamoja hivyo kipindi cha chaguzi kinapofika kisiwe sababu za kutoleana lugha chafu zitazowqvunja heshima, baada yake waendelee upendo kwani zoezi hilo likiisha itakuwa vigumu kwenda kuombanaradhi.

"Sisi wana UWTwote ni wamoja tumeendelea kufanyakazi kwa upendo, hivyo niwaombe tunapokwenda katika mchakato wa uchaguzi tukaendeleze upendo wetu, hakuna haja ya kumtolea mwingine lugha isiyofaa, kwani baada uchaguzi tutapata wakati mgumu wa kuombana msamaha," amesema Mkali

Katibu wa UWT wilaya hiyo, Catherine Makungwa, amewashukuru wabunge, mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Taifa, Mariam Ulega na madiwani kwa michango yao mikubwa katika vipindi vyote kwa kusaidia UWT kufanikisha shughuli mbalimbali.

"Tunawashukuru wabunge wetu Muharami Mkenge (Bagamoyo), Ridhiwani Kikwete (Chalinze), wakiwemo wa Viti Maalumu, Hawa Mchafu, Dkt. Harris na Subira Mgalu ambao katika vipindi vyote wamekuwa nasi usiku na mchana, wakiwemo wadau mbalimbali," amesema Makungwa.

Kwa upande wao madiwani wa viti maalumu wanaomaliza muda wao, wamesoma taarifa zao za utekelezaji katika kipindi cha miaka mitano, huku Debora Rashid na Veronica Ndetiyai wakiwakaribisha wana UWT kuwania nafasi hiyo kwani kila mtu ana haki ya kugombea.

"Hii nafasi ni ya wote nitumie fursa hii kuwakaribisha kugombea Viti Maalumu katika Tarafa ya Msoga, kwani kila Mwanachama ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa," alisema Debora.
Katibu wa UWT wilaya hiyo, Catherine Makungwa
Sekretarieti ya UWT Wilaya ya Bagamoyo
Wajumbe

Wajumbe wakifuatilia


No comments