Masjid Hamduun Kibwende yaandaa sherehe ya Idi
Mohamed Mwaraha
Na Omary Mngindo, Mlandizi
MASJID Hamduun Bin Mansuur iliyopo Kitongoji cha Kibwende Kata ya Mlandizi Kibaha Vijijini Pwani, imeandaa sherehe maalumu ya kusomwa na kutafsitiwa kwa Kitabu Kitakatifu cha Mwenyeezimungu.
Hafla hiyo itayofanyika sikukuu ya Idi Mfungo Tatu itashirikisha wanaMadrasa wapatao 60 chuoni hapo, itayoanzia mchana mpaka jioni huku vijana wakitaraji kuonesha uwezo wao wa kusoma na kutasfiri kitabu hicho.
Hayo yamebainishwa na Mohamed Mwaraha Mwenyekiti wa Kamati ya muda ya kuelekea shughuli hiyo, ambapo alisema kuwa wapo katika maandalizi kati ya uongozi ukishirikiana na wazazi na walezi.
"Kumekuwepo na utamaduni siku za sikukuu watoto wanakuwa na uhuru wa kwenda kuburudika katika kumbi au maeneo yasiyosalama, huko kuna vitendo vinavyosababisha mmomonyoko wa maadili," Mwaraha.
Mwaraha aliongeza kuwa "Lengo kubwa ni kuona watoto wanaondokana na tabia zisizokuwa za maadili, kwani wanapokwenda kwenye maeneo hayo wanakutana na vishawishi vya aina tofauti," alisema Mwaraha.

Shaibu Idi
"Tumeshakaa vikao zaidi ya viwili vinavyolenga kufanikisha azma hiyo, tunawaomba wazazi wa wanafunzi na wa madhehebu mengine tuungane katika kufanikisha malengo ya kuwajengea malezi bora watoto wetu," alisema Ustadhi Idi.
Madarasa hiyo inayomilikiwa na Kampuni ya Animal Feed inayojihusisha na utengenezaji wa vyakula vya mifugo, imekuwa mkombozi katika eneo ilo ambapo wanafunzi wanasomeshwa bila kulipia ada.
No comments