Header Ads

ad

Breaking News

Sekretarieti ya Maadili yapata mafanikio makubwa kutumia mifumo ya TEHAMA

Kamishna wa Maadili Jaji Sivangirwa Mwengesi akifungua kikao kazi cha Sekreterieti ya Maadili na Wahariri jijini Dar es Salaam, Ijumaa Mei 30,2025

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KAMISHNA wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi, amesema taasisi za umma zinatakiwa kutumia mifumo ya TEHAMA ili kutekeleza sera ya serikali mtandao.

Amesema kwa upande wao wamejipanga kutekeleza sera hiyo, na tayari wamepiga hatua kubwa ya uboreshaji majukumu yao kwa mfumo huo wa teknolojia hiyo mpya.

Kamishna huyo alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao kazi kati ya Tume ya Maadili na Wahariri wa habari kilichofanyika leo Ijumaa Mei 30, 2025 jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mafanikio ya Tume hiyo, Jaji Mwangesi amesema kupitia mifumo hiyo wanapokea kwa urahisi matamko kuhusu mali na madeni ya watumishi wa umma, hivyo ni hatua kubwa ya maboresho ya utendaji kazi, hata kuchangia kupunguza adha na gharama kwa wadau wanaokwenda kupata huduma Tume ya Maadili.

Amesema kuwa, hatua hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuboresho ya utendaji wa Tume ya Maadili, kwani imekuwa ikiwajali wadau na kuwapunguzia usumbufu na gharama ya kwenda katika ofisi za Tume hiyo.

“Mfumo huu umeanzishwa ili kutekeleza sera ya Serikali mtandao, ambapo Serikali imeagiza taasisi zote za umma kutumia mifumo ya TEHAMA kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano na kuboresha utendaji.” amesema Jaji Mwangesi.

Naye, Katibu Msaidizi wa Idara ya Ukuzaji Maadili wa tume hiyo, Fabian Pokela amesema kuwa, pamoja na taasisi hiyo kuwa na dhamana, suala la utawala bora, suala la uadilifu kwa viongozi na uadilifu katika utumishi wa umma, ni suala mtambuka, si suala linalopaswa kushughulikiwa na taasisi moja.

Katibu Msaidizi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Fabian Pokela akitoa wasilisho lake

"Tunapopewa dhamani ya kusimamia maadili ya viongozi ni kwasababu ya dhamana tu waliyonayo, lakini wote tuna maslahi kwenye suala la mabadiliko ya viongozi wetu nchini, kwa hiyo maslahi haya ambayo ni ya kwetu sote, kwasababu uadilifu huu ndiyo unaochangia utendaji bora, ndiyo unaochangia mambo yaende vizuri kwa ajili ya maendeleo yetu sote, hasa kwa viongozi," amesema Pokela.

Amewataja waandishi wa habari kutafakari kama wana habari nafasi yao nini kwenye suala la uadilifu kwa viongozi, kwani upande mmoja utawatazama kama Sekretarieti ya Maadili ya viongozi waliopewa hiyo dhamana, kwani kila taasisi imepewa dhamana yake, hivyo si jukumu alilopewa mwingine ni lake peke yake, wakati mwingine wanajisahau.

Amesema serikali imetengeneza mkakati wa taarifa dhidi ya rushwa, ambapo hivi sasa wako awamu ya nne ya utekelezaji, hivyo lengo la tano la mkakati huo ambao unapaswa kutekelezwa na kila mtanzania, ni kuhakikisha sekta za umma na sekta zisizo za umma zinashirikishwa katika juhudi hizo za rushwa na kukuza uadilifu nchini.

"Majukumu yanayotekelezwa na Sekretarieti ya Maadili  ni pamoja na kupokea matamko yanayotolewa na viongozi wa umma, lengo likiwa kuongeza uwajibikaji wa viongozi wa umma katika kutunza rasirimali za umma na kudhibiti mgongano maslahi," amesema.

Ameongeza kuwa, lengo lingine ni  kusaidia rasilimali za umma kunufaisha umma na si kwa maslahi binafsi. Pokela ametaja aina tano za matamko ya viongozi ambayo ni maslahi, rasilimali na madeni, zawadi, kutopoteza sifa za kuchaguliwa au kuteuliwa, maslahi katika maamuzi, maslahi katika mikataba na serikali na mgongano wa maslahi.

Ameongeza kuwa, Tume hupokea na kushughulikia malalamiko ya ukiukwaji wa maadili, ambalo lengo lake ni kutoa fursa ya kusikiliza malalamiko ya wananchi pamoja na kushirikisha taasisi nyingine kutatua malalamiko.

"Tume hufanya uchunguzi wa malalamiko ili kuthibitisha ukweli wa tuhuma dhidi ya viongozi na kuchukua hatua za kuwafikisha mbele ya baraza la maadili."


















No comments