Wasichana 82 wa Chibok, waachiwa huru na Boko Haram
![]() |
Wasichana 21 walioachiwa huru Oktoba 2016 |
Wasichana hao ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi wanafunzi 270 waliotekwa nyara kutoka shule ya malazi katika mji wa Chibok ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Wasichana hao wote 82 kwa sasa wanalindwa na jeshi la Nigeria mahali salama, baada ya kuletwa kwa barabara kutoka maeneo ya ndani kabisa vijijini, hadi katika kambi ya jeshi ya Banki, karibu na mpaka na Cameroon, hayo ni kwa mjibu wa mwaandishi habari wa BBC Stephanie Hegarty kutoka Lagos.
Utekaji nyara huo ambao ulifahamika baadaye kama "Chibok girls" ulisababisha kilio kikubwa kote duniani na kampeini za kutaka waachiwe huru ikatanda kote katika mitandao ya kijamii.
Kabla ya hatua hii ya hivi punde ya kuwaachia wasichana hao, inakisiwa kuwa zaidi ya wasichana 195 wangali hawajulikani waliko.
Idadi ya washukiwa wa Boko Haram ambao wameachiwa huru na utawala wa Nigeria, bado haijajulikana.
No comments