Real Madrid yaifuta Juventus fainali ya Klabu Bingwa Ulaya
Mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Ulaya, Real Madrid imetinga fainali ya michuano hiyo baada ya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-2, lakini katika mechi iliyopigwa usiku wa kuamkia leo imechapwa mabao 2-1.
Bao la kwanza la Atletico lilifungwa dakika 12 na Saul Niguez, kabla ya Antoine Griezmann kuipatia bao la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 16.
Mabao hayo yaliizindua Real Madrid ambapo dakika ya 42, ilijipatia bao lake lililofungwa na Isco, bao lililowamaliza nguvu wenyeji wa mchezo huo waliokuwa wakicheza mbele ya mashabiki wao kwenye Uwanja wa Estadio Vicente Calderon jijini Madrid.
Kwa ushindi huo, Real Madrid wataumana na Juventus ya Italia iliyoiondosha Monaco ya Ufaransa kwa jumla ya mabao 4-1.
Saul Niguez wa Atletico Madrid akiruka juu zaidi ya Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
Antoine Griezmann akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la pili kwa mkwaju wa penalti.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema akionesha ufundi wake kwa kuwatoka mabeki watatu wa Atletico Madrid katika mchezo wa nusu fainali Klabu Bingwa Ulaya uliopigwa usiku wa kumakia leo jijini Madrid.
Kiungo wa zamani wa Malaga, Isco akimfunga kipa Jan Oblak baada ya kupangua mpira uliopigwa na Kroos ndani ya meta sita.
Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia ushindi dhidi ya Atletico Madrid usiku wa kuamkia leo. Madrdi pamoja na kufungwa mabao 2-1, lakini imesonga mbele kwa jumla ya mabao 4-2.
Karim Benzema wa Real Madrid akiunganisha kwa kichwa mpira wa krosi uliopigwa na Marcelo.
Kocha wa Atletico, Diego Simeone akishangaa
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane akifuatilia mchezo wa timu yake dhidi ya Atletico Madrid.
Mashabiki wa Real Madrid wakishangilia ushindi.
No comments