JIJI LA ARUSHA LANUFAIKA NA MIRADI YA BARABARA, ELIMU NA AFYA .
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo afungua barabara ya Mahakama – St. James wakati wa ziara yake Jijini hapa. |
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (mbele) akikagua ujenzi wa kituo cha Afya Muriet. |
![]() |
Jiwe la Msingi lililowekwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwenye barabara ya Mahakama – St. James |
………………
Jiji la Arusha lina Mtandao wa barabara zenye urefu wa Km 334 na kati ya hizo barabara za Lami ni Km 86.7 tu na zilizobakia ni Changarawe pamoja na barabara za udongo. Tangu Halmashauri hii ilipopata hadhi ya kuwa Jiji imeanza kutekeleza mkakati wa ujezi wa barabara za Lami kila mwaka wa Fedha kwa kutumia mapato ya ndani.
Halkadhalika Halmashauri imeendelea kutafta miradi kutoka Tamisemi na Mfuko barabara ili kuongeza mtandao wa barabara za Lami pamoja na changarawe kufanya mji huu kuendana na hadhi ya Jiji.
Mwaka wa Fedha 2016/2017 Halmashauri imeendelea na kazi ya uboreshaji wa miundombinu kwa kujenga barabara za Lami atika Maeneo ya Mahakamani – Kaloleni (0.65Km), Unga Ltd – Muriet (5.9 Km), Bp – Sunflag –Njiro (0.85) ambazo zote zimegharmu zaidi Tsh Bil 7 kutoka Mapato ya ndani, Mfuko wa barabara pamoja na Mradi wa Tscp.
Miradi yoyte ta barabara imefunguliwa, kukaguliwa na kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa ziara yake iyokamilika mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo pia aliweza kufungua barabara ya Oljoro Kisimani iliyojengwa kwa kiwango cha changarawe (4 Km) pamoja na Ujenzi wa Daraja la Oljoro.
Kupitia ziara hiyo Mhe. Gambo ameweza kufungua madarasa 17 kwa niaba ya madarasa 60 ya Shule za Msingi yaliyojengwa, madarasa 7 kwa niaba ya madarasa 15 ya Sekondari na kutembelea ujenzi wa vituo vya Afya 2 maeneo ya Muriet na Moshono ambavyo vyote ujenzi wake umeanza kwa mwaka huu wa Fedha
No comments