Yanga mambo bado
Kwa vile wajumbe kadhaa wa Kamati ya
Utendaji ya Yanga akiwemo Mwenyekiti wa kamati hiyo Lloyd Nchunga wamejiuzulu,
Kamati ya Uchaguzi ya Yanga imeliandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) ikitaka mwongozo juu ya hilo.
Kwa kuzingatia hilo, TFF imepeleka
suala hilo kwa kamati yake ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ili itoe
maoni yake kisheria ya nini kinafanyike kuhakikisha Yanga inaendelea na
shughuli zake kama kawaida.
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi
za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana leo
jioni kushughulikia suala hilo na baadaye Kamati ya Uchaguzi ya Yanga pamoja na
Kamati ya Uchaguzi ya TFF zitapewa maelekezo ya kufanya kwa kuzingatia taratibu
zilizopo.
No comments