TWIGA STARS KWENDA ETHIOPIA ALHAMISI
![]() |
Twiga Stars |
Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga
Stars) inatarajia kuondoka nchini Mei 24 mwaka huu kwa ndege ya Ethiopian
Airlines kwenda Addis Ababa kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Fainali za Afrika
kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia. Mechi hiyo itachezwa Mei 27 mwaka huu.
Msafara wa Twiga Stars utakuwa na
watu 25 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Mwenyekiti wa Chama
cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Lina Kessy ndiye
atakayeongoza msafara huo.
Twiga Stars itarejea nyumbani Mei 28
mwaka huu kusubiri mechi ya marudiano itakayochezwa Juni 16 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam. Mshindi ndiye atakayepata tiketi ya kucheza Fainali za
Nane za AWC zitakazochezwa Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
No comments