MALAWI YATUA KUIVAA TAIFA STARS
Timu ya Taifa ya Malawi (The Flames)
inatarajiwa kuwasili nchini leo saa 10 jioni kwa ndege ya Air Malawi kwa ajili
ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayofanyika Jumamosi (Mei 26 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Mechi hiyo ni kwa ajili ya kuipima
nguvu Taifa Stars kabla ya mechi yake mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika
dhidi ya Ivory Coast itakayofanyika Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan. Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini chini ya Kocha
Kim Poulsen.
Malawi itafikia hoteli ya Sapphire
iliyoko Mtaa wa Lindi na Sikukuu ambapo Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa
sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh.
15,000 VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.
Malawi ambayo itafikia hoteli ya
Sapphire iliyoko Mtaa wa Lindi na Sikukuu baada ya mechi hiyo itakwenda
Zanzibar ambapo Mei 28 mwaka huu itacheza na Zanzibar Heroes.
Makocha wa timu zote mbili Taifa
Stars na The Flames kesho (Mei 25 mwaka huu) saa 5 asubuhi watakuwa na mkutano
na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF.
No comments