JUMLA ya makocha 24 kutoka nchi mbalimbali, wamejitokeza
kuomba kazi ya kufundisha klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, nafasi iliyoachwa
wazi na Mserbia Kostadin Bozidar Papic.
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu amaeiambia BIN ZUBEIRY mchana
huu kwamba, makocha waliojitokeza ni kutoka Uholanzi, Scotland, Serbia na Ujerumani .
Sendeu alisema wengine wanatokea England na Ureno anakotokea Cristiano Ronaldo.
Sendeu alisema Kamati ya Ufundi bado inapitia wasifu wa makocha
hao kabla ya kupendekeza watatu wa kuingia kwenye mchujo wa mwisho, ambao miongoni
mwao atapatikana kocha mpya wa Yanga.
Aidha, Sendeu alisema kwamba Kamati ya Utendaji ya Klabu ya
Yanga, imeahairisha Mkutano wake na Wazee, ili kushughulikia mambo mengine yaliyojitokeza ikiwa ni
pamoja na mapendekezo ya Yussuf Manji.
No comments:
Post a Comment