Thursday, May 17, 2012

BREAKING NYUZZZZZZZ! MAFISANGO AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI






Soka la Tanzania limegubikwa na majozi kufuatia taarifa za kufariki dunia kwa kiungo wa mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Patrick Mafisango Mutesa usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa Mafisango alifariki Dunia maeneo ya Chang'ombe Veta wakati akirejea nyumbani kwake.

Kamwaga alisema kuwa wamestushwa sana na taarifa za kifo cha mchezaji wao tegemeo ambaye hivi karibuni alitoa mchango mkubwa sana wakati timu hiyo ikishiriki katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Amesema kuwa japo wapo katika maombolezo, taarifa zaidi zitatolewa mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo kabla ya saa tano asubuhi ya leo (Mei 17).

"Hili ni pigo kubwa kwa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Rwanda kwani hivi karibuni tu kocha mkuu wa timu hiyo, Milutin Sredojovic 'Micho'  alimjumuisha mareemu Mafisango katika kikosi cha wachezaji 32 wa kikosi hicho kinachojiandaa kwa ajili ya kutafuta tiketi ya kucheza Kombe la Dunia," alisema Kamwaga.

Marehemu Mafisango amekaa nje ya timu ya taifa ya Rwanda "Amavubi Worriors" kwa takribani mwaka mmoja na kiwango chake cha juu kilimvutia sana Micho ambaye alikuja kuona pambano la watani wa jadi dhidi ya Yanga na Simba kushinda mabao 5-0.

No comments:

Post a Comment