![]() |
Abidal |
BARCELONA, Hispania
BEKI wa klabu ya Barcelona, Eric
Abidal, ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kufanyiwa matibabu ya ini mwezi.
Abidal mwenye miaka 32, alithibitisha
kuhitaji kufanyia matatibu ya kupandikizwa ini mapema mwaka huu, yapata mwaka
baada ya kutakiwa kufanyiwa upasuaji wa ini.
Taarifa fupi ya Barcelona ilisema:
"Beki huyo mfaransa alitolewa hospitali jana baada ya kupandikizwa ini
Aprili 10, mwaka huu.
"Daktari wa timu alieleza kuwa,:
'Nilipewa taarifa za maendeleo yake yanavyokwenda. Abidal ataendelea kuripoti
hospitali kwa uchunguzi mara kwa mara.'"
Kufuatia upasuaji wake wa kwanza
Machi 2011, Abidal alikuwa nje kwa muda wa wiki saba, alirejea mwishoni na
kucheza baadhi ya mechi akitokea kwenye benchi.
No comments:
Post a Comment