Na Omary Mngindo, Mlandizi
KITUO kinachotoa huduma ya Elimu kwa watoto kuanzia miaka miwili na kuendelea cha Zegeleni Day Care kilichopo Zegeleni Kata ya Visiga Kibaha Pwani, kuanzia January 2026 itapeleka wanafunzi 50 katika shule ya Innovate.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa kituo hicho Neema Mwambila, akizungumza na Fahari News katika shule ya Awali na Msingi ya Innovate, baada ya tamasha la michezo lililofanyika shuleni hapo.
Alisema kuwa anatambua ubora wa elimu kutoka katika shule hiyo, ambapo kwa mara ya kwanza alimpeleka mwanafunzi mmoja ambae amekuwa na kiwango kizuri, hivyo kumshawishi kuwapeleka wengine wataoingia Darasa la kwanza mwakani.
George Ndaki akizungumza na waandishi wa habari"Kutokana na ubora wa elimu inayopatikana hapa Innovate nimevutiwa nayo, nimepanga mwakani kuanzia Januari watoto 50 wataoanza Darasa la kwanza watakuja kusoma hapa," alisema Mwambila.
Akizungumza baada ya hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Innovate George Ndaki alianza kumshukuri Mkurugenzi mwenzake kwa uamuzi huo, huku akieleza kwamba wamejipanga kikamilifu katika uboreshaji wa elimu.
"Tuna miundombinu ya kutosha itayotufanikishia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaoendelea kujiunga, wito kwa wanaKibaha Vijijini na waTanzania kwa ujumla walete watoto wao Innovate wapate elimu bora," alisema Ndaki.
Aliongeza kuwa "Tuna vyumba vya madarasa yenye kukidhi upatikanaji wa elimu boraena sio bora elimu, hapa kuna walimu waliobobea katika ufundishaji nawaomba Wazazi wenzangu wakiwemo walezi watumie fursa hii," alimalizia Ndaki.
No comments:
Post a Comment