Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia wananchi wa Kata ya Masumbwe,katika viwanja vya Shule ya Msingi Masumbwe, Ijumaa Septemba 5,2025 wilayani Mbogwe, Mkoa wa Geita .
Dkt Nchimbi ameingia mkoani Geita kuendelea na Mikutano yake ya Kampeni ya kusaka kura za ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akitokea mkoani Shinyanga.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Nchimbi aliwanadi wagombea ubunge akiwemo mgombea ubunge wa Jimbo la Mbongwe, Fagasoni Nkingwa na madiwani.
Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya kampeni mkoani Geita ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.
No comments:
Post a Comment