Wednesday, September 10, 2025

DKT.NCHIMBI AZIDI KUINADI ILANI YA UCHAGUZI MKUU KATAVI

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Maridadi, Mpanda mjini mkoani Katavi


Na Mwandishi Wetu, Katavi

MGOMBEA Mwenza wa Urais wa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ameendelea kunadi Ilani ya chama hicho ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.

Dkt.Nchimbi jana Septemba 9,2025 aliwasili mkoani Katavi na kuhutubia wananchi katika Uwanja wa Maridadi, Mpanda mjini, kwenye mkutano wake wa hadhara wa Kampeni akitokea mkoani Rukwa.

Baada ya kuwahutubia wananchi wa Mpanda Mjini, Balozi Nchimbi alianadi wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali ya m koa huo,akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mpanda mjini, Haidary Sumry pamoja na madiwani.

Awali, Dkt Nchimbi amewahutubia wananchi wa Majimoto,katika Jimbo la Kavuu mkoani Katavi na kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Laurent Luswetula pamoja na madiwani.

Akiwa katika mkutano huo Dkt.Nchimbi ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea urais wa CCM, Dkt.Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.















No comments:

Post a Comment