Header Ads

ad

Breaking News

DKT.NCHIMBI AMNADI KOOLA, MADIWANI JIMBONI VUNJO, AMPONGEZA DKT.KIMEI

Na Mwandishi Wetu, Vunjo

MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amewahutubia Wananchi wa kata ya Himo,jimbo la Vunjo katika uwanja wa Polisi Himo Wilayani ya Vunjo,akiendelea na mikutano yake ya Kampeni leo Jumamosi Septemba 13,2025 mkoani Kilimanjaro.

Baada ya kuwasalimia Wananchi hao,Dkt Nchimbi ambae ni mgombea mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,pia alitumia nafasi hiyo kuwanadi Wagombea Ubunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Vunjo,Ndugu Enock Zadock Koola pamoja na Madiwani.

Dkt.Nchimbi ambae ameingia Kanda ya Kaskazini,akianzia mikutano yake ya Kampeni Mkoani Arusha na sasa ameingia mkoa wa Kilimanjaro kusaka kura za ushindi wa Kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.


Ngombea mwenza huyo amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.

Wanachama wa CCM wa jimbo hilo wamepongezwa na Dk Nchimbi wakiwemo waliotia nia ya kugombea ubunge akisema anashukuru kutokuwa na mpasuko baada ya kumalizika zoezi la uteuzi ndani ya chama hicho.

Dk Nchimbi pia amempongeza aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dk Charles Kimei akimsifia kwa kuendele kukipigania chama cha CCM kwa kuwaombea kura Rais Samia, mbunge wa jimbo hilo na madiwani.










No comments