Mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo, Dkt. Nchimbi amepokewa na wazee na viongozi wa kimila wa Jamii ya Wachaga (Mangi) na kumvalisha mavazi ya Kimila na kusimika kuwa mlezi wa Machifu wa Wilaya ya Mwanga.
Baada ya tukio hilo Dkt.Nchimbi ambae ni mgombea mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,aliwahutubia Wananchi hao na baadae aliitumia nafasi hiyo kuwanadi wagombea ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea ubunge wa Jimbo la Mwanga, Ngwaru Maghembe na madiwani katika jimbo hilo.
Dkt.Nchimbi ambae yuko Kanda ya Kaskazini,anaendelea na miikutano yake ya Kampeni mkoa wa Kilimanjaro kusaka kura za ushindi wa Kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Ngombea mwenza huyo amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.
No comments:
Post a Comment