Header Ads

ad

Breaking News

𝐌𝐂𝐇𝐄𝐍𝐆𝐄𝐑𝐖𝐀: 𝐓𝐔𝐌𝐄𝐈𝐍𝐔𝐀 𝐒𝐄𝐊𝐓𝐀 𝐘𝐀 𝐀𝐅𝐘𝐀 𝐑𝐔𝐅𝐈𝐉𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐀𝐒𝐈 𝐊𝐔𝐁𝐖𝐀

Na Mwandishi Wetu, Rufiji

“𝘉𝘪𝘯𝘢𝘥𝘢𝘮𝘶 𝘴𝘪𝘺𝘰 𝘬𝘸𝘢 𝘢𝘫𝘪𝘭𝘪 𝘺𝘢 𝘮𝘢𝘭𝘪, 𝘮𝘢𝘭𝘪 𝘯𝘥𝘪𝘺𝘰 𝘬𝘸𝘢 𝘢𝘫𝘪𝘭𝘪 𝘺𝘢 𝘣𝘪𝘯𝘢𝘥𝘢𝘮𝘶.” – 𝐌𝐰𝐚𝐥𝐢𝐦𝐮 𝐉𝐮𝐥𝐢𝐮𝐬 𝐊. 𝐍𝐲𝐞𝐫𝐞𝐫𝐞

Kauli hii ya Baba wa Taifa inapata maana yake halisi leo hii tunaposhuhudia mabadiliko makubwa katika sekta ya afya Jimbo la Rufiji chini ya uongozi wa 𝗠𝗵𝗲. 𝗠𝗼𝗵𝗮𝗺𝗺𝗲𝗱 𝗠𝗰𝗵𝗲𝗻𝗴𝗲𝗿𝘄𝗮, Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika kipindi cha uongozi wake wa miaka kumi, Mhe. Mchengerwa amefanikisha mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya, hatua iliyogusa maisha ya maelfu ya wananchi wa Rufiji.

Akizungumza na wananchi, Mhe. Mchengerwa alisema:

“𝑻𝒖𝒍𝒊𝒌𝒖𝒘𝒂 𝒏𝒂 𝒗𝒊𝒕𝒖𝒐 𝒗𝒊𝒕𝒂𝒕𝒖 𝒕𝒖 𝒗𝒚𝒂 𝒂𝒇𝒚𝒂 𝒂𝒎𝒃𝒂𝒗𝒚𝒐 𝒉𝒂𝒗𝒊𝒌𝒖𝒘𝒂 𝒏𝒂 𝒖𝒘𝒆𝒛𝒐 𝒘𝒂 𝒌𝒖𝒕𝒐𝒂 𝒉𝒖𝒅𝒖𝒎𝒂 𝒔𝒕𝒂𝒉𝒊𝒌𝒊. 𝑵𝒅𝒂𝒏𝒊 𝒚𝒂 𝒎𝒖𝒅𝒂 𝒎𝒇𝒖𝒑𝒊 𝒏𝒊𝒎𝒆𝒋𝒆𝒏𝒈𝒂 𝒗𝒊𝒕𝒖𝒐 𝒗𝒊𝒑𝒚𝒂 𝒗𝒚𝒂 𝒂𝒇𝒚𝒂 𝒕𝒊𝒔𝒂, 𝒏𝒂 𝒖𝒋𝒆𝒏𝒛𝒊 𝒖𝒏𝒂𝒆𝒏𝒅𝒆𝒍𝒆𝒂 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂 𝒎𝒂𝒆𝒏𝒆𝒐 𝒎𝒃𝒂𝒍𝒊𝒎𝒃𝒂𝒍𝒊. 𝑲𝒘𝒂 𝒎𝒂𝒓𝒂 𝒚𝒂 𝒌𝒘𝒂𝒏𝒛𝒂 𝑹𝒖𝒇𝒊𝒋𝒊, 𝒕𝒖𝒏𝒂𝒑𝒂𝒕𝒂 𝒌𝒊𝒕𝒖𝒐 𝒄𝒉𝒂 𝒂𝒇𝒚𝒂 𝒄𝒉𝒂 𝒈𝒉𝒐𝒓𝒐𝒇𝒂 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂 𝑲𝒂𝒕𝒂 𝒚𝒂 𝑼𝒎𝒘𝒆 𝒄𝒉𝒆𝒏𝒚𝒆 𝒕𝒉𝒂𝒎𝒂𝒏𝒊 𝒚𝒂 𝒛𝒂𝒊𝒅𝒊 𝒚𝒂 𝒃𝒊𝒍𝒊𝒐𝒏𝒊 2.5. 𝑨𝒊𝒅𝒉𝒂, 𝒌𝒖𝒕𝒐𝒌𝒂 𝒌𝒖𝒘𝒂 𝒏𝒂 𝒛𝒂𝒉𝒂𝒏𝒂𝒕𝒊 𝒎𝒐𝒋𝒂 𝒑𝒆𝒌𝒆𝒆, 𝒔𝒂𝒔𝒂 𝒕𝒖𝒎𝒆𝒇𝒂𝒏𝒊𝒌𝒊𝒔𝒉𝒂 𝒖𝒋𝒆𝒏𝒛𝒊 𝒘𝒂 𝒛𝒂𝒉𝒂𝒏𝒂𝒕𝒊 42 𝒌𝒂𝒕𝒊𝒌𝒂 𝒗𝒊𝒋𝒊𝒋𝒊 𝒗𝒚𝒐𝒕𝒆 𝒗𝒚𝒂 𝑾𝒊𝒍𝒂𝒚𝒂 𝒚𝒂 𝑹𝒖𝒇𝒊𝒋𝒊.”

Mageuzi haya yameimarisha huduma za afya kwa wananchi, ambapo sasa huduma za tiba zinapatikana karibu zaidi na vijiji, bila wananchi kulazimika kusafiri Dar es Salaam au maeneo mengine kutafuta huduma.

Mapinduzi haya ya sekta ya afya yanakwenda sambamba na mapinduzi ya fikra, kwa kuwa jamii yenye afya njema ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli.

Kwa kazi kubwa iliyokwisha kufanyika na dhamira ya kuendeleza jitihada hizi, Mhe. Mohammed Mchengerwa anawaomba wananchi wa Jimbo la Rufiji kumpa ridhaa tena ili aendelee kuliletea taifa hili maendeleo.

No comments