Header Ads

ad

Breaking News

DKT. NCHIMBI ATIA MGUU MWANZA KUOMBA KURA KUELEKEA UCHAGUZI

Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

MGOMBEA Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi, amewasili mkoani Mwanza leo Agosti 29, 2025 kwa ajili ya kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.

Balozi Dkt Nchimbi anatarajia kufanya mikutano mbalimbali kwa ajili ya kuzinadi sera pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya 2025-2030. CCM kimeingia siku ya pili za kampeni zake baada ya jana kuzinduliwa rasmi hapo jana jijini Dar es Salaam na Mgombea Urais Dkt.Samia Suluhu Hassan.






No comments