Header Ads

ad

Breaking News

WCF yalipa fidia wafanyakazi 19,650, yazoa tuzo

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt.John Mduma akiwasilisha wasilisho lake kwa wahariri na waandishi wakati wa kikao kazi kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakaziu (WCF), Dkt.John Mduma amesema katika muda wa miaka 10 tangu kuanzishwa kwa mfuko huo, wamelipa Fidia wafanyakazzi na wategemezi wao 19,650.

Taasisi hiyo ya hifadhi ya jamii iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Fidia kwa wafanyakazi Na.20 ya mwaka 2008, ilianza kutekelezwa rasmi Julai 1,2015 imefanikiwa kuwalipa waliopata ajali, kuugua au kufariki kutokana na kazi.

Akizungumza katika kikao kazi kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam, kilichowahusisha wahariri na waandishi wa Habari kwa uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, amesema taasisi hiyo hivi sasa imeongeza idadi ya mafao hadi kufikia saba.

Ameyataja mafao hayo ni fao la matibabu (bila kikomo), fao la ulemavu wa muda mfupi, fao la ulemavu wa kudumu, fao la pensheni kwa wategemezi, fao la wasaidizi wa mgonjwa, fao la utengano na fao la msaada wa mazishi.

WCF ambao wapo chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), kwa mujibu wa sheria ya Msajili wa Hazina Na.370 na marekebisho yake na sheria nyingine zinazoongoza Ofisi ya Msajili wa Hazina, kazi na wajibu wa ofisi hiyo zimegawanywa katika makundi matatu.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa, WCF hutoa ulinzi wa kijamii kwa wafanyakazi wote walioko katika sekta ya umma na binafsi dhidi ya madhara yanayotokana na ajali, magonjwa au vifo vinavyotokea kazini au kutokana na kazi.

Ameongeza kuwa, mafanikio ya WCF yamechangiwa na miaka minne ya uongozi a Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, amba;po wametekeleza mapinduzi ya kidijitali, kwani aidi ya asilimia 90 ya huduma zao zote zinatekelezwa kwa njia ya mtandao.

"Mifumo hii ya kidijitali imepunguza sana urasimu, zaidi umeongeza  uwazi na kuboresha ufanisi wa utendaji kazi na hata kuchangia kwa kiasi kikubwa mwaka 2024 kupata cheti cha ithibati cha ISO kwa utoaji huduma bora kwa viwango vya kimataifa," amesema Mkurigenzi Mkuu Dkt.Mduma.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano kwa Umma na Mawasiliano Sabato Kosuri akizungumza katika kikao kazi

Dkt.Mduma ameongeza kuwa, mwaka 2023, Mfuko huo ulipata tuzo ya kimataifa ya  International Social Security Association (ISSA) kwa matumizi mazuri ya Teknolojia ya Habari na mawasiliano (TEHAMA).

"Mwaka 2025 Mfuko wetu ulishika nafasi ya pili katika tuzo za serikali Mtandao (eGa Award) na nafasi ya tatu kqwenye TEHAMA Award 2025, kwa taasisi za umma zilizofanikiwa kuondoa urasimu kupitia TEHEMA."

Dkt.Mduma amesema lengo kubwa la Mfuko huo ni kuwekeza  vitega uchumi mbalimbali ili upate rasilimali ambazo zitawezesha kuwa na uendelevu wa kulipa Fidia kwa wanachama wake.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa, WCF wanaendelea na kampeni mbalimbali za elimu na uhamasishaji kwa waajili na wafanyakazi juu ya haki zao, taratibu za fidia na usalama mahali pa kazi, ambayo imesaidia kupunguza ajali na magonjwa kazini, pamoja na kuongeza usajili wa waajiri.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bakari Kimwanga akitoa neno la shukrani

"Pamoja na mafanikio yote, zi[pom changamoto wanazoendelea kuzifanyia kazi ikiwemo waajiri kutojisajili na kutowasilisha michango kwa wakati," amesema.

"Wapo waajiri ambao hawajatekeleza matakwa ya sheria ya kuwasajili wafanyakazi na kuwasilisha michango kila mwezi, hivyo hunyima haki ya wafanyakazi wanapopatwa a majanga kazini," amesema Mkurugenzi Mkuu huyo.

Ameongeza kuwa, wataendelea kuboresha huduma na kushirikiana na wadau wote, Pamoja na kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi ili kila mfanyakazi anapopatwa na madhila, anapata haki yake kwa wakati.

Amewataka waajiri wote sekta ya umma na binafsi kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria, na kwa wafanyakazi kuendelea kufanyakazi kwa bidi, wakijua kwamba mfuko wao uko imara na thabiti kuwahudumia.




Mnufaika wa mfuko
Mnufaika wa mfuko





No comments