Tushirikiane kuelimisha umma manufaa ya Soko la Bidhaa Tanzania-Mkurugenzi
MKURUGENZI Mtendaji wa Soko la Biashara Tanzania (TMX), Godfrey Malekano, amewataka wahariri kushirikiana kwa karibu na soko hilo ili kuelimisha zaidi umma manufaa na ubora wake.
Kauli hiyo aliitoa Septemba 7,2023, wakati alipozungumza na wahariri kuhusu shughuli na faida za soko hilo kwa jamii.
Alisema Soko la Bidhaa ni mfumo rasmi unaokutanisha wauzaji na wanunuzi kwa pamoja na kufanya biashara ya mikataba ya bidhaa, inayotoa uhakika wa ubora, ujazo na malipo.
"Soko hili huleta wanunuzi wengi wa ndani na nje ya nchi ambao sio lazima wafike kwenye soko la bidhaa au nchini kwa kuwa mauzo katika Soko la Bidhaa hufanyika kwa kutumia mfumo wa kidijitali ambao huwawezesha wanunuzi wa bidhaa kufanya manunuzi popote walipo ndani na nje ya nchi,"amesema.
“Soko la Bidhaa litaendelea kufanya utafiti kwa kushirikiana na wadau husika ili kuongeza bidhaa zaidi.
“Soko la Bidhaa litaendelea kushirikiana na waandishi wa habari kwani, kupitia wao ni rahisi kuufikia umma wa watanzania," amesema.
Kwenye semina hiyo fupi iliyoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, amesema utafiti ni sehemu ya jukumu muhimu kwa TMX katika kutekeleza majukumu yake.
“Kazi ya kujenga mfumo imara wa Soko la Bidhaa inategemea mchango wa serikali, taasisi na sekta binafsi hivyo, ushirikiano ni muhimu sana kufikia adhima hiyo,” amesema.
No comments