BABA MZAZI WA LWANDAMINA AFARIKI
![]() |
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina |
Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mzambia, George Lwandamina, amekumbwa na msiba mzito baada ya baba yake mzazi kufariki.
Lwandamina ambaye amejiunga na
Yanga Novemba, mwaka jana, amempoteza baba yake huyo aliyekuwa
akisumbuliwa na maradhi ya kupooza ambapo amefariki usiku wa Jumanne
August 29, 2017.
Lwandamina amesema: “Kutokana na
msiba huo, natarajia kuondoka leo August 31 kwenda nyumbani Zambia kwa
ajili ya mazishi na nikifika ndio tutajua tunazika lini kwani nasubiriwa
mimi tu nifike.
“Baba alikuwa anasumbuliwa na
maradhi ya kupooza na amefariki Jumanne usiku, nikienda huko nitakaa
mpaka kila kitu kimalizike na natarajia kurudi Jumamosi ya wiki ijayo.”
Fullshangweblog.com inaungana na
wanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania kumtakia pole George Lwandamina
na familia yake kwa kuondokewa na mpendwa wao pamoja na mashabiki wa
Yanga kwa ujumla
No comments