Askofu wa kanisa Katoliki awapa hifadhi wanamgambo wa kikristo wenye silaha, wakipiga kambi katika Seminari moja Jamhuri ya Afrika ya Kati-CAR
![]() |
Wanamgambo wa kikristo wenye silaha, wakipiga kambi katika Seminari moja Jamhuri ya Afrika ya Kati-CAR. (CATHOLIC BISHOP OF BANGASSOU, JUAN JOSÉ AGUIRRE MU) |
Ameiambia BBC kwamba, maisha ya wakimbizi hao yamo ''hatarini'' kutoka kwa waasi wenye silaha wa kundi la Balaka.
The UN's humanitarian chief warned last week of possible genocide.
Wiki iliyopita, afisa mkuu wa umoja wa mataifa wa kitengo cha utoaji msaada wa kibinadamu, alitoa tahadhari ya uwezekano wa kutokea mauwaji ya kimbari.
Stephen O'Brien, amesema kuwa vurugu inazidi kuongezeka huku hali ikiwa mbaya zaidi nchini humo.
"Vurugu inaongezeka na kuhatarisha hali ya usalama, huku kukiwa na uwezekano wa kutokea kwa maafa zaidi hata kuliko ilivyokuwa miaka minne iliyopia."
Ameongeza kuwa: "tahadhari ya awali ya kutokea kwa mauwaji ya kimbari ipo. Lazima hali hii ikabiliwe sasa na haraka iwezekanavyo." alisema O`Brien.
Makundi ya kukabiliana na lile la Balaka "yanayojilinda" yaliundwa lakini pia yamelaumiwa kwa mauwaji ya kiholela.
Jina Balaka ni jina la mtaani linalomaanisha risasi, kwa hivyo jina la kikundi hicho lina maana kuwa "Wale wanaosimamisha risasi". Na kwa upande mwingine jina la Seleka, lina maanisha, "muungano" hiyo ni kutokana na kabila la Sango, linalozuingumzwa pakubwa nchini humo.
Kundi moja lililo na silaha, linalokabiliana na lile la Balaka liliundwa, na limeshutumiwa kwa mauwaji mabaya ya watu.
BBC
No comments