![]() |
Diego Costa na kocha Antonio Conte |
Paris Saint-Germain wanajiandaa kuzungumza na Barcelona kuhusu uhamisho wa pauni milioni 196 wa Neymar, 25. (Guardian)
Barcelona wanapanga kuzungumza na Monaco kuhusu kumsajili Kylian Mbappe, 18. Barca wanatarajia kupata fedha za kutosha kumsajili Mbappe baada ya kumuuza Neymar, 25. (Daily Mail)
Chelsea wanataka pauni milioni 44 kutoka kwa Atletico Madrid kwa ajili ya Diego Costa, 28, baada ya kukamilisha usajili wa Alvaro Morata, 24, kutoka Real Madrid. (Independent)
Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo amesema hakuna uhakika thabiti iwapo Diego Costa atakwenda Atletico Madrid. (Mirror)
Liverpool wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22, baada ya dau la pauni milioni 66 kukataliwa. (Mirror)
West Ham wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier 'Chicharito' Hernandez, 29, kutoka Bayer Leverkusen. (Sky Sports)
Arsenal wamewaambia West Ham kuwa watalazimika kutoa pauni milioni 20 ikiwa wanamtaka kiungo Jack Wilshere, 25. (Daily Star)
Paris Saint-Germain wamemtuma mkurugenzi wao wa michezo kwenda London kujaribu kumshawishi Alexis Sanchez, 28, ambaye pia anasakwa na Manchester City. (Sun)
Everton wamepata matumaini zaidi ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30. (The Telegraph)
Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa Real Madrid Danilo, 26, kwa pauni milioni 26.5. (Guardian)
Manchester city wanakaribia kukamilisha usajili wa beki Benjamin Mendy, 23, kutoka Monaco. (Times)
Manchester United wanahusishwa na kutaka kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain, Marco Verratti, 24, baada ya mchezaji huyo kumfanya Mino Raiola kuwa wakala wake mpya. (Sun)
Inter Milan wamewaambia Manchester United lazima wamjumuishe Anthony Martial, 21, katika mkataba wowote utakaohusu uhamisho wa Ivan Perisic, 28. (Independent)
AC Milan wamesema kiungo mshambuliaji wao Suso, 23, anayenyatiwa na Tottenham, hauzwi. (Tuttomercato)
PSG watamuuza kiungo Blaise Matuidi, 30, iwapo dau zuri litatolewa. (L'Equipe)
No comments:
Post a Comment