RAIS MAGUFULI KUFANYA ZIARA MKOANI SINGIDA KESHO, ATAZINDUA BARABARA YA ITIGI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (Picha ya Maktaba).

Mkuu wa Mkoa
wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) juu ya ugeni wa Rais Magufuli Mkoani Singida siku ya
kesho.

Sehemu ya Barabara ya Manyoni-
Itigi-Chaya itakayozinduliwa kesho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Mkuu wa
Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Pius Luhende wakati wa maandalizi ya
mapokezi ya Rais Magufuli.
………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi
Mkoani Singida kesho Julai 25 ambapo atazindua barabaraya
Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3.
Akizungumza na waandishi wa habari
mapema leo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amesema Rais
Magufuli anatarajiwa kufanya uzinduzi wa barabara hiyo katika eneo la
NjiaPanda, Itigi na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.
“Napenda kuwataarifu wananchi wote
kuwa rais wetu Mpendwa atatuzindulia barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya,
hivyo basi tujitokeze tukamshukuru kwakutuletea maendeleo wana Singida,
ametufanyia jambo kubwa sana, shukrani zetu hiyo kesho pale njiapanda
zitaendelea kumpa hamasa ya kutuletea maendeleo zaidi” amesema Dkt
Nchimbi.
Dkt Nchimbi ameongeza kuwa
wananchi wajitokeze kumlaki na kutoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa
kuokoa rasilimali za nchi hasa katika sekta ya madini ambayo Mkoani
Singida pia yanapatikana kwa wingi na kwakuwa jitihada hizo zimelenga
kuwanufaisha wana Singida na watanzania wote.
“Rais Magufuli ameokoa rasilimali
nyingi za taifa na anapambana usiku na mchana kuzilinda ili watanzania
hasa wanyonge wafaidike, wengi tumekuwa tukifurahishwa sana na jitihata
hizo, hivyo basi kesho tuonyeshe upendo wetu na shukrani zetu kwake”,
ameongeza Dkt Nchimbi.
Aidha amesema barabara
itakayozinduliwa kesho na Rais Magufuli ni kiunganishi muhimu kati ya
Mkoa wa Singida na Tabora na hivyo kurahisha usafirishaji tofauti na
ilivyokuwa kabla ya kujengwa, pia itarahisisha kwa wasafirishaji wa
mikoa ya Singida na maeneo ya jirani kuelekea Mkoa wa Tabora mpaka
Kigoma.
No comments