Mrisho Gambo azindua sensa ya watu,mifugo na makazi wilayani Ngorongoro

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
………………………………………………………………………….
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo amezindua sensa ya watu,mifugo na makazi katika kata ya
Ngorongoro ambayo kwa sehemu kubwa ipo ndani ya hifadhi ya mamlaka ya
Ngorongoro ikiwa ni maagizo ya waziri mkuu Kassim Majaliwa aliyoyatoa
mwezi Desemba 2016 katika ziara yake mkoani Arusha.
Akizungumza na wananchi wa tarafa
hiyo Kaimu Mkurugenzi wa takwimu za Uchumi toka Ofisi ya Takwimu ya
Taifa Bi Joy Sawe amesema lengo ni kujua kiasi cha shughuli za
kibinaadamu katika eneo hilo ili serikali iweze kupanga mipango yake ya
kiuchumi kwa usahihi. Pia amesema wao kama ofisi ya Takwimu ya Taifa
wanawashukuru sana wananchi wa Tarafa hiyo kwa ushirikiano wanaowapa
kwani hii ni mara yao ya kwanza kuendesha zoezi kama hili, hivyo
mafanikio ya zoezi hili yatawapa uzoefu mkubwa kuliendesha katika maeneo
mengine.
Naye Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Bw. Rashid Mfaume Taka amewataka
wananchi wa tarafa hiyo kuendelea kuwapa wataalamu hao ushirikiano
kwani zoezi hili lina manufaa makubwa kwao, na pia baada ya zoezi hili
wajiandae kwa zoezi la uwekaji alama mifugo ambalo litasimamiwa na
wanakijiji wenyewe ili kuwaondoa hofu wananchi hao.
Akizungumza na wananchi hao Mhe.
Gambo amewaambia wananchi hao hawana haja ya kua na hofu na serikali yao
kwani ina lengo zuri katika kuboresha maisha yao na ustawi wa mamlaka
ya Ngorongoro.
“Nyinyi wenyewe ni mashahidi wa namna ambavyo hifadhi hii ya mamlaka ya Ngorongoro inavyojitoa katika kuboresha maisha yenu, lengo la sensa hii ni kujua ni wakazi kiasi gani na mifugo kiasi gani iko eneo hili kwani kuna baadhi watu ambao sio wakazi halali wa eneo hili wamekuja na mifugo hali ambayo ina hatarisha ustawi wa hifadhi yetu” alisema Gambo.
“Nyinyi wenyewe ni mashahidi wa namna ambavyo hifadhi hii ya mamlaka ya Ngorongoro inavyojitoa katika kuboresha maisha yenu, lengo la sensa hii ni kujua ni wakazi kiasi gani na mifugo kiasi gani iko eneo hili kwani kuna baadhi watu ambao sio wakazi halali wa eneo hili wamekuja na mifugo hali ambayo ina hatarisha ustawi wa hifadhi yetu” alisema Gambo.
Pia amewaonya wale wote ambao
wanaweka siasa katika kila jambo, ” yeyote atakayekwamisha zoezi hili
namuhakikishia tutahangaika nae hakuna siasa katika zoezi hili” alionya
Mhe. Gambo.
Zoezi hili litafanyika kwa muda
wa siku kumi na linafanywa na vijana 138 wa tarafa hii ambao wamepewa
mafunzo ya kutumia dodoso la kieletroniki katika ukusanyaji wa taarifa
No comments