Mbunge Tundu Lissu anyimwa dhamana, arudishwa rumande
DAR ES SALAAM- MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemnyima dhamana Mbunge wa Singida
Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, katika kesi ya uchochezi
inayomkabili kiongozi huyo.
Aidha, kesi hiyo
ambayo imesikilizwa kwa mara ya kwanza leo, imeahirishwa hadi Julai 27 mwaka
huu.
Katika kesi hiyo,
Lissu alikuwa akiwakilishwa na jopo la mawakili 21 wakiongozwa na Fatma Karume
na Peter Kibatala, wakati upande wa Serikali ukiwakilishwa na mawakili watano.
No comments