Manchester United yailaza Manchester City debi ya ugenini
Romelu Lukaku na Marcus Rashford wakisherehekea ushindi wa mabao yao. (Manchester United FC)
Manchester United
imejipatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao wa jadi
Manchester City katika debi ya kwanza ugenini huku ziara za 2017
zinazofadhiliwa na Aon zikiendelea kuipatia ushindi The Red Devils.
Kikosi hicho cha Jose Mourinho kilianza kwa mashambulizi huku Anders Herrera akianzisha juhudi hizo mapema, huku mashambulio mengine yakitoka nje ya eneo la hatari, United wakimjaribu kipa mpya wa City Ederson.
David De Gea alilazimika kuwa macho katika upande mwengine huku Raheem Sterling akishambulia mara mbili , kabla ya Chris Smalling kuzuia mashambulizi mawili yaliofanywa na Patrick Roberts na Sterling.
United hata hivyo ilifanikiwa dakika nane kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza baada ya Lukaku kupata pasi muruwa kutoka kwa Paul Pogba na kucheka na wavu.
Dakika mbili baadaye, Marcus Rashford aliifungia United bao la pili akifunga baada ya kazi nzuri kutoka kwa Henrikh Mkhitaryan. BBC
No comments