Friday, July 21, 2017

Mahakama yatupilia mbali rufaa ya Tigo, yaamuliwa kuwalipa AY na FA bilioni 2/-

FA-AY-pic
Ambwene Yessayah ‘AY’ na Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’
 Breaking News:
Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali rufaa iliyofunguliwa na kampuni ya Tigo kupinga kuwalipa wasanii AY na MwanaFA Tshs 2,185,000,000 kwa kutumia nyimbo zao bila kulipa.


Wakili Albert Msando ambaye anawakilisha wasanii hao amesema huu ni ushindi muhimu kwa sanaa ya Tanzania. Amenukuliwa akisema "ni haki yao kulipwa kwa sababu ni kazi zao ambazo zinalindwa kisheria".

Mei 12, 2016 
Awali, mahakama ya Hakimu Mkazi Ilala jijini Dar es Salaam, iliiamuru kampuni ya mawasiliano ya Tigo kuwalipa wasanii Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Ambwene Yessayah ‘AY’ jumla ya sh. bilioni 2.18 baada ya kutumia kazi zao za muziki bila ridhaa yao.

Hukumu hiyo imetolewa kutokana na kampuni hiyo kutumia kazi za wasanii hao ‘Dakika Moja’ na ‘Usije Mjini’ kama miito ya simu bila makubaliano yoyote. Hiyo inakuwa hukumu kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwenye historia ya mambo ya ukiukwaji wa haki miliki za kazi za ubunifu na sanaa nchini.

Hakimu mkazi wa mahakama ya Ilala, Juma Hassan alitoa hukumu hiyo Jumatano hii kufuatia mvutano mahakamani kati ya pande hizo mbili uliodumu kwa kipindi cha miaka minne. Pia Tigo imetakiwa kulipa shilingi milioni 25 nyingine kama sehemu ya fidia.

Taarifa za kesi hiyo zimefahamika wiki hii baada ya wakili wa mastaa hao Alberto Msando kupost kwenye Instagram picha akiwa nao kwenye mahakama kuu jijini Dar es Salaam.

Kampuni hiyo ilikuwa imepeleka pingamizi la hukumu hiyo ya mahamaka ya hakimu mkazi Ilala katika mahakama kuu ya Tanzania. Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa Jumanne hii lakini imeahirishwa hadi Ijumaa.

Madai ya Mwana FA na AY ni kuwa Tigo ilitumia kazi zao bila kuwa na mkataba nao wowote au kampuni ya kati iliyowawakilisha na hivyo kuingiza fedha ambayo wawili hao wanaamini ni nyingi.
Awali walitaka walipwe fidia ya shilingi bilioni 4.3.

No comments:

Post a Comment