Kiongozi wa upinzani Zambia alalamikia mazingira mabaya gerezani
Hakainde Hichilema alikamatwa baada ya msafara wake kukataa kuupisha ule wa rais. (AFP)
Kiongozi wa
upinzani nchini Zambia aliye korokoroni Hakainde Hichilema, amefikisha
siku 100 gerazani tangu akamatwe akilalamikia mazingira mabaya yaliyo
gerezani.
Anakabiliwa na mashtaka uhaini kufuatia kisa hicho.
Bwana Hichilema ambaye kwa sasa anazuiliwa katika gereza lenye ulinzi mkali, aliandika kwenye mtandao wake wa Facebook kuwa hana chuki na yeyote
Alisema mapenzi yake ni kuona mabadilko nchini Zambia.
"Tunaamini kuwa licha ya wafungwa hawa kufanya makosa, wanahitaji kuhudumiwa kwa njia ya kibinadamu," alisema hichilema.
No comments