Kata ya Kigoma kuwapa mitaa nyota za zaman waliocheza Mataifa ya Afrika 1980
![]() |
Zitto Kabwe, Mbunge Kigoma mjini |
Wachezaji na makocha wote watapata mitaa kwenye eneo la Mji Mwema.
Namshukuru Sana Diwani wa Kata ya Kigoma Ndugu Hussein Haidary Kalyango Kwa kufanikisha hili. Nitajithidi wachezaji wote waliohai na walimu wao wahudhurie shughuli maalumu ya kuzindua mitaa yenye majina yao.
Kata hii pia imetoa jina Kwa Prof. Abdulrahman Mohamed Babu kwa mchango wake kwenye umajumui wa Afrika na ukombozi wa Afrika.
Kikosi cha Taifa Stars ya mwaka 1980 hiki hapa:
Athumani Mambosasa
Juma Pondamali
Taso Mutebezi
Jelah Mtagwa
Leodgar Tenga
Mohamed Kajole
Husein Ngulungu
Mtemi Ramadhan
Juma Mkambi
Omari Hussein
Mohamed Masewa
Thuweni Ally
Peter Tino
Ahmed Thabit
Charles Boniface
Salim Amiri
Adolf Richard
Zamoyoni Mogela
Martin Kikwa
George Kulagwa
Uzinduzi wa Mitaa Hii ya Mashujaa wetu utafanyika Juumamosi ya Kwanza ya Mwezi wa Tisa ambapo kutachezwa Mechi kati ya Timu ya Manispaa ya Lake Tanganyika SC na Timu ya Bukavu Dawa ya DRC.
Zitto Kabwe
Kigoma Mjini
No comments