Jeshi la Polisi lawauwa wahalifu wawili Kibiti
![]() |
Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Liberatus Sabas |
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua watu wawili
wanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika
Kanda maalumu ya kipolisi Rufiji ambapo mmoja kati ya watu hao
ametambulika kwa jina la Abdallah Ally Ngande Makeo ambaye alikuwa
akitafutwa na Jeshi la Polisi kwa muda mrefu kutokana na kushiriki
kwake katika matukio ya mauaji maeneo ya Ikwiriri, Kibiti pamoja na
uvamizi wa kituo cha Polisi Ikwiriri.
Akielezea tukio hilo, Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la
Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema kuwa tukio
hilo lilitokea mnamo tarehe 19, julai, 2017 saa mbili usiku katika eneo
la Utende kata ya Ikwiriri, wilaya Rufiji kanda maalum ya Polisi
Rufiji.
“Askari Polisi wa doria waliwatilia mashaka watu
wanaokadiliwa kuwa watano ambapo walipoanza kuwafutilia ndipo walianza
kukimbia huku wakiwashambulia askari kwa risasi.
“Askari nao kwa ujasiri walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi wahalifu wawili miongonio mwao ambao baadaye walifariki wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya muhimbili kutokana na kuvuja damu iliyosababisishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata” alisema Sabas.
Aliongeza kuwa katika eneo hilo la tukio ilipatikana silaha moja
aina ya rifle 375 ambayo ilikutwa imekatwa kitako na mtutu ikiwa na
risasi mbili (2). Aidha, Miili ya marehemu wote wamehifadhiwa katika
chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa ya muhimbili.
Kamanda sabas ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea
kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zitakazosaidia
kukamatwa wahalifu wengine waliosalia na kwamba opereheni hiyo ya
kuwasaka wahalifu katika Kanda hiyo ya kipolisi Rufiji ni endelevu na
hakuna atakayebaki.
No comments