Jaribio la kifaa kinachowalinda wanawake dhidi ya HIV lafaulu
Watafiti nchini Marekani wanasema kuwa jaribio ambalo vijana wa Marekani walitumia mviringo kujilinda na virusi vya HIV limefanikiwa. (GETTY IMAGE)
Watafiti nchini
Marekani wanasema kuwa jaribio ambalo vijana wa Marekani walitumia mpira
wa mviringo kujilinda na virusi vya HIV limefanikiwa.
Wasichana walitumia mviringo wa plastiki uliowekwa dawa za kujilinda na Ukimwi, ambao hubadilishwa kila mwezi baada ya kipindi cha miezi sita.
Ni mojawapo ya mipango ya kutengeneza kifaa ambacho wanawake watatumia kujilinda dhidi ya maambukizi ya HIV ili wasiweze kuwategemea wanaume kuvaa mipira ya kondomu.
Wakiripoti ugunduzi huo mpya kuhusu virusi vya HIV mjini Paris, watafiti walisema kuwa wanafurahi kwamba wasichana hao walitumia mviringo huo na kusema kuwa wameupenda.
Wanawake na wasichana walio kati ya umri wa miaka 15-24 wanadaiwa kuwa moja kwa tano ya visa vyote vya maambukizi ya HIV duniani.
Takriban wanawake 1,000 huambukizwa virusi kila siku katika Afrika ya Jangwa la Sahara.
No comments