Thursday, July 20, 2017

Guardiola akataa kumpiga bei Aguero

                                                 Kocha wa Man City, Pep Guardiola 
 
KOCHA Mkuu wa timu ya Manchester City, Pep Guardiola amesema hana mpango wa kumpiga bei mshambuliaji wake, Sergio Aguero Kun.


"Ni mchezaji wetu na atabakia hapa,"alisema Guardiola wakati akizungumzia tetesi za mchezaji huyo huenda akaondoka.

Hata hivyo kocha huyo amesema wanahitaji kusajili wachezaji wengine watatu au wanne katika kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.

Man City imekua kwenye mawindo ya kuwania saini za walinzi Danilo wa Real Madrid na Benjamin Mendy anayekipiga na katika timu ya Monaco, pamoja na mshambuliaji hatari wa Arsenal Alexis Sanchez. BBC

No comments:

Post a Comment