Mjane wa aliyekuwa
rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela Graca Machel, amesema atamshtaki
daktari wake bwana Mandela, kutokana na taarifa alizochapisha kwenye
kitabu kuhusu siku za mwisho za Mandela.
Radio ya taifa nchini Musumbiji ilitangaza taarifa iliyotolewa na wakfu wa Bi Machel ikilaani kitabu hicho vikali.
Bi Machel alisema kuwa kitabu hicho kinakiuka heshima ya bwana Mandela.
Kitabu hicho kimeandika taarifa kuhusu siku za mwisho kabla ya kifo cha Mandela.
Kimetaja kutokuwepo kwa maelewano kati ya madaktari na familia ya Mandela.
Bi Mandela anasema kuwa kitabu hicho kilikiuka siri iliyo kati ya daktai na mgonjwa.
No comments:
Post a Comment