GLOBAL EDUCATION LINK YAFANYA UDAHILI WA PAPO KWA PAPO KWA VYUO VIKUU VYA NJE
Mkurugenzi
wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel wa (kwanza kushoto)
akizungumza na wateja waliofika kupata huduma katika ofisi za Global
Education Link zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es
Salaam.
Afisa
Masoko wa Global Education Link (GEL) Damaricy Peter wa (kwanza
kushoto) akiwapa maelekezo wateja waliofika kupata huduma katika ofisi
za Global Education Link zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar
es Salaam.
Afisa
wa Hati ya Kusafiria Passport , Abdul Milanzi akimsainisha fomu ya hati
ya kusafiria mteja wa Global Education Link GEL leo katika ofisi za
Global Education Link zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es
Salaam.
Meneja
Masoko wa Chuo Kikuu cha Lovely Professional, Love Kumas (kulia)
akizungumza na mteja katika ofisi za Global Education Link (GEL) leo
jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
…………………………………………………………………………..
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Baada
ya Matokeo ya Kidato cha Sita , Global Education Link (GEL) ambao ni
mawakala wa Vyuo Vikuu vya Nje imesema kuwa wanafunzi wanaotaka
kujiunga na vyuo vikuu vya nje udahili ni papo kwa papo na vyuo hivyo
viko wazi.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education
Link (GEL), Abdulmalik Mollel amesema katika azma ya serikali ya awamu
ya tano ya viwanda, inahitaji rasilimali watu ya kutosha ambao ndio
watasukuma gurudumu hilo la viwanda na ujuzi upo katika vyuo vya nje
ambapo nchi zenye vyuo vina uatajiri wa viwanda.
Mollel
amesema kuwa vyuo ambavyo anashirikiana na vina uwezo wa
kutosha katika uzalishaji wa rasilimali watu katika sekta ya viwanda.
Amesema
kuwa wazazi wanaotaka kupeleka wanafunzi katika vyuo vikuu vya
nje hawatajutia kutokana na mazingira wanayokwenda kusoma huko.
Mollel
amesema kuwa wazazi na wanafunzi wafike katika ofisi zao ziko katika
mikoa ya Dar es Salaam viwanja vya Saba saba , Dodoma , Mbeya, Mwanza,
Zanzibar, Arusha pamoja na nchi ya Zambia.
Amesema
kuwa mwanafunzi atayekuwa anapitia katika wakala hiyo atapata uangalizi
kwa muda wote masomo yake katika kuhakikisha mzazi kile anachokifanya
kwa kijana wake hawezi kujutia.
Mollel
amesema kuwa wazazi na wanafunzi wanaweza kufika katika ofisi zao kwa
maelezo na jinsi kuwafanyia udahili wa papo kwa papo.
No comments