Benki ya NMB yafungua matawi mapya mikoa mitatu


Mkuu wa Wilaya Igunga –John
Mwaipopo (kati kati ) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya NMB
Nkinga katika wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora wengine pichani ni Meneja
wa NMB kanda ya Magharibi Leon Ngowi (wa kwanza kushoto) na Meneja wa
NMB tawi la Nkinga Jasmina Tengia (kulia). Tawi hili ni miongoni mwa
matawi mengine mawili yaliozinduliwa kwa pamoja katika kanda ya
magharibi mwishoni mwa wiki.
Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB imezidi kung’ara
nchini huku ikifanikiwa kutanua mtandao wake kwa kufungua matawi mapya
matatu katika mikoa ya Kigoma, Tabora na Simiyu. Uzinduzi wa matawi hayo
ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo kufunguliwa kwake
kutaleta neema kwa wakazi wa maeneo hayo.
Mkoani Kigoma benki hiyo ilizindua
tawi jipya Wilaya ya Uvinza, Tabora (Igunga) katika mji wa mashuhuri wa
Nkinga na Simiyu Wilaya mpya ya Itilima.
Awali akizungumza katika uzinduzi
wa tawi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, Mwanamvua
Mrindoko, aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kutumia fursa ya benki hiyo
ikiwemo kuhifadhi fedha zao na huduma za kifedha ikiwemo mikopo nafuu
inayotolewa na benki hiyo.
Alisema hatua ya kuzinduliwa kwa
tawi hilo la Benki la NMB sasa ni wazi wilaya hiyo itajikwamua kiuchumi
ikiwemo wananchi wake kujenga urafiki na benki hiyo kwa kupata huduma
bora za kifedha.
“Kuzinduliwa kwa tawi hili jipya
katika Wilaya yetu ya Uvinza sasa ni kielelezo kwamba wananchi wataweza
kujikwamua kiuchumi kwa kuwa na urafiki wa karibu na benki ikiwemo
kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa,” alisema Mrindoko.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Igunga Mkoani Tabora, John Mwaipopo, akizinduwa tawi jipya katika mji wa
Nkinga alisema ni kielelezo tosha cha wilaya hiyo kupiga hatua
kimaendeleo. Aidha akifafanua zaidi kwa wananchi waliojitokeza kwenye
uzinduzi huo, Mwaipopo alisema hatua hiyo ni ishara nzuri na wananchi
wataweza kutumia fursa kidekede zinazotolewa na benki hiyo.
“Asanteni NMB kwa kufika hapa
Nkinga, awali wananchi walikuwa wakitembea umbali mrefu hadi Igunga
mjini kutafuta benki lakini sasa huduma za kifedha zitapatikana hapa
kupitia benki hii nzuri na bora kutokana na huduma zake,” alisema
Mwaipopo.
Naye Meneja wa TRA Wilaya ya
Nzega, Adolf Mtumbuka, akizungumza katika uzinduzi huo, alisema tawi
hilo litasaidia kukusanya mapato ya Serikali ambapo awali wananchi wa
Nkinga walilazimika kwenda makao makuu ya wilaya.
“Ninapenda sana kuishukuru Benki
ya NMB sasa imekuja kufungua milango ya kiuchumi katika eneo hili la
Nkinga ambalo lipo Wilaya ya Igunga lakini pia lipo jirani sana na
Wilaya ya Nzega. Hivyo kuzinduliwa kwake kutasaidia kukusanya mapato ya
Serikali kupitia benki hii ambao pia hukusanya mapato ya Serikali kwa
niaba ya TRA,” alisema Mtumbuka.
Kutokana na kuimarisha huko kwa
mtandao wa benki hiyo Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Benson
Kilangi, alisema kuzinduliwa kwa tawi hilo kutachochea wananchi
kuzalisha vizuri na fedha watakazopata watahifadhi benki.
“Tunahitaji kuweza ndani ya Wilaya
ya Itilima ili wananchi wapate muda wa kutosha katika shughuli za
uzalishaji ili kuondokana na umaskini. Hivyo nawaomba wananchi wa
Itilima mtumie fursa hii ya Benki ya NMB kwa kisingizio hamna mitaji au
hajui mfanyaje.
No comments