WAJUMBE WA BARAZA LAAWAKILISHI WAELIMISHWA KUHUSU HOMA YA INI

Waziri wa Afya Mahmoud Thabit
Kombo akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika mkutano
wa kushajihisha wajumbe hao kuhusu kifua kikuu, ukimwi na homa ya ini
katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.

Spika wa Baraza la Wawakilishi
Zubeir Ali Maulid ambae alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo akiufungua
rasmi katika Hoteli ya Ocean View (kulia) Mnadhimu wa Baraza Ali Salim
Haji na (kushoto) Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa kuwashahishaji kuhusu
Kifua kikuu, Ukimwi na homa ya Ini uliofanyika Hoteli ya Ocean View
Kilimani Mjini Zanzibar.

Mratibu wa huduma za homa ya Ini
Zanzibar Dkt. Sania Shafi akiwaelezea Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
hali halisi juu ya homa ya Ini katika mkutano uliofanyika Hoteli ya
Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.

Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi akitoa mchango katika mkutano huo.

Meneja Kitengo Shirikishi Kifua
kikuu, Ukimwi na homa ya Ini Dkt. Farhat Ahmed akijibu maswali ya
wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika mkutano wa kuwashajihisha kuhusu
maradhi hayo katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga.
………………………………………………………….
Na Ramadhani Ali – Maelezao Zanzibar
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
wameshtushwa na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na homa ya Ini wakati
wananchi wengi hawana uelewa juu ya maradhi hayo na Serikali haijaandaa
mikakati imara ya kupambana nayo.
Wajumbe hao walieleza hisia zao
wakati wakichangia mada ya hali halisi ya homa ya Ini katika mkutano wa
kushajihisha wajumbe hao kuhusu maradhi ya Kifua kikuu, Ukimwi na Homa
ya Ini ulioandaliwa na Kitengo Shirikishi cha maradhi hayo katika Hoteli
ya Ocean View Kilimani.
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni
Rashid Makame Shamsi alisema wakati homa ya Ini inaongoza kwa
kusababisha vifo vingi zaidi ikilinganisha na maradhi mengine
haikuzungmzwa katika Bajeti ya mwaka huu ya Wizara ya Afya.
Amesema kukosekana taarifa ya
homa Ini ndani ya Bajeti ya Wizara huku wananchi hawana uelewa juu ya
homa hiyo itapelekea kuenea kwa kasi na kupoteza maisha ya wananchi.
Mwakilishi wa kuteuliwa Ahmada
Yahya ameishauri Wizara ya Afya kupitia Kitengo Shirikishi kutoa taaluma
zaidi kwa wananchi ili kuwa na uelewa mpana wa homa ya Ini na njia za
kujikinga nayo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi
ambae alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo ameishauri Kamati ya Bajeti ya
Baraza hilo kuangalia uwezekano wa kukipatia fedha Kitengo Shirikishi
cha Ukimwi, Kifua Kikuu na homa ya Ini ili kiweze kukabiliana nayo.
Mratibu wa huduma za homa ya Ini
Zanzibar Dkt. Sania Shafi aliwafahamisha wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi kuwa homa hiyo ni janga kama yalivyo maradhi ya Ukimwi na
Kifua kikuu hivyo mashirikiano ya pamoja yanahitajika katika kukabiliana
nayo.
Aliwaeleza wajumbe hao kuwa njia
kuu za maambukizi ya homa ya Ini ni sawa na zile za maambukizi ya Virusi
vya Ukimwi lakini virusi vya homa ya Ini vinakasi zaidi.
Alisema mtu anapopata homa ya Ini
hupoteza uwezo wa kufanyakazi kwa vile Ini linaharibika na
husababisha kupata saratani na hatimae kupoteza maisha.
Aliwashauri vijana kujiepusha
kufanya vitendo vinavyosababisha kupata Virusi vya Ukimwi kwa vile
maradhi hayo yanauhusiano mkubwa na homa ya Ini.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kupitia Wizara ya Afya kwa kufahamu athari ya homa ya Ini
inaendelea kufanya tafiti na hivi karibu itafungua kliniki katika
hospitali kuu ya Mnazimmoja kwa ajili kushughulikia homa hiyo.
No comments