DC Kishapu aongoza sherehe za Mazingira
Mkuu wa wilaya ya Kishapu,
Nyabaganga Talaba akiangalia alizeti kwenye banda la Halmashauri ya wilaya hiyo
wakati wa sherehe hizo.
|
Mkuu wa wilaya ya Kishapu,
Nyabaganga Talaba akiwa na viongozi wengine wakimsikiliza mtalaamu kuhusu
majiko yasiyotumia kuni wakati akitembelea mabanda.
|
Ofisa Kilimo kata ya
Ngofila, Genes Tarimo (kushoto) akiwapa maelezo kuhusu madumu maalumu vya
kuchemshia maji ya kunywa mgeni rasmi na viongozi aliombatana nao.
|
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniface Butondo akizungumza wakati wa sherehe hizo. |
Ofisa kutoka Mgodi wa
Williamson Mwadui akitoa maelezo kwa wageni kuhusu jiko linalotumia sola
kupikia vyakula mbalimbali bila kutumia kuni wala mkaa.
|
Sehemu ya vitalu vya miche
vikiwa katika banda la maonesho vikiwa tayari kwa ajili ya kuonesha wananchi
namna ya kupandwa.
|
Wananchi wakitembelea
banda la halamashauri ya wilaya ya Kishapu.
|
Mkuu wa wilaya ya Kishapu,
Nyabaganga Talaba (wa pili kushoto) akionesha furaha yake kwa kuserebuka na
kwaya ya wanafunzi.
|
Mwandishi Wetu, Kishapu
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ametumia Siku
ya Mazingira Duniani kuwaagiza viongozi katika ngazi mbalimbali kutoa elimu kwa
wananchi kuhusu athari zinazotokana na vitendo vya ukataji miti.
Ametoa agizo hilo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba
yake na Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba leo wakati wa kilele cha
siku hoyo kilichofanyika kimkoa kata ya Mwamashele wilayani hapa.
Amesema kuwa wananchi wengi hawaelewi kuwa tunapokata
miti kwa wingi tunatishia uhai wetu na wa wanyama hali inayotokana na ukosefu
wa mvua na hivyo kusababisha ukame.
Telack amesema kuwa misitu ndiyo mhimili mkubwa wa
kulinda mazingira yetu na kutupatia nishati, dawa za asili, vifaa vya ujenzi
pamoja na kuboresha hali ya hewa.
“Pamoja na muhimu wa misitu kwa binadamu na mazingira
imekumbwa na uharibifu mkubwa katika mkoa wetu wa Shinyanga kwa matumizi
mbalimbali yakiwemo ya uchomaji mkaa,” anasema.
Ameongeza kuwa uchomaji wa mkaa katika maeneo mengi
kama vile Nyasamba umekuwa kama shughuli ya kujipatia kipato na hivyo kutishia
kutoweka kwa misitu.
Amewataka wadau kutumia nishati mbadala kama vile
vinyeshi vya wanyama na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi hayo kwani
matumizi ya mkaa ni adui wa mazingira.
Mkuu huyo wa mkoa ameonya kuwa uchomaji mkaa na
utumiaji wake huongeza hewa ya ukaa na kusababisha mabadiliko ya tabia ya nchi
na hatimaye kuleta ukame.
“Hivyo ni vema wananchi
tubadilike na tuachane na matumizi ya rasilimali zetu kuwa endelevu kwa kupanda
miti zaidi ili tuhifadhi ardhi, vyanzo vya maji na kuboresha hali ya hewa,”
anasema.
Sherehe hizo zilihudhuriwa
pia na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine
Matiro, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniface Butondo,
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga,
wakurugenzi wa halmashauri za Ushetu, Msalala, Shinyanga na Kahama.
Sherehe hizo ambazo
kitaifa zilifanyika jana mkoani Mara zinachagizwa na kaulimbiu ya Hifadhi ya
Mazingira ni muhimili kwa Tanzania ya Viwanda.
No comments