REAL MADRID, BARCELONA KASI NI ILE ILE LIGI KUU HISPANIA
![]() |
Wachezaji wa Real Madrid wakipongezana baada ya kupata bao dhidi ya Deportivo la Coruna usiku wa kuamkia leo kwenye Uwanja wa Estadio Municipal de Riazor. Real Madrid ilishinda mabao 6-1. |
![]() |
Alvaro Morata akiifungia Real Madrid bao dhidi ya Deportivo La Coruna katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Estadio Municipal de Riazor usiku wa kuamkia leo. Real Madrid ilishinda mabao 6-1. |

James Rodriguez wa Real aliifungia timu yake bao la pili.

Lucas Vazquez aliiongezea timu yake ya Real Madrid bao la tatu katika mchezo huo wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya Deportivo La Coruna usiku wa kuamkia leo. Real Madrid iliibuka na ushindi wa mabao 6-1.

James Rodriquez akifunga bao dhidi ya katika mechi dhidi ya Deportive la Coruna usiku wa kuamkia leo.
James Rodrigues alifunga mabao mawili, Alvaro Morata, Lucas Vazquez, Isco na Casemiro kila mmoja aliipatia timu yake bao moja na kuwahakikishia mashabiki wao waliosafiri na timu furaha wakati wote wakiwa ugenini.
Deportivo ilijipatia mabao mawili kupitia Florin Andone na Joselu, lakini hayakuwasaidia kubakiza pointi tatu katika uwanja wao wa nyumbani wa Estadiop Municipal de Riazor.

Roberto Torres aliifungia bao Osasuna kwa mkwaju wa adhabu.

Gomes akishangilia bao lake.

Messi akishangilia moja ya mabao aliyofunga usiku wa kuamkia leo kwa shuti kali la umbali wa meta 20.

Paco Alcacer aliyeingia kuchukua nafasi ya Messi akimtoka beki wa Osasuna Oier Sanjurjo na kuifungia timu yake bao la tano.

Javier Mascherano alifunga bao lake la kwanza akiitumikia Barcelona, baada ya miaka saba akiwa na klabu hiyo kwa mkwaju wa penalti.

Alcacer wa Barcelona akimpita kipa Sirigu na kufunga bao la tano.
Barcelona wao waliifunga Osasuna mabao 7-1, mechi iliyowapa aibu kubwa wachezaji wa kikosi hicho cha Osasuna iliyopigwa Uwanja wa Camp Nou mini Barcelona.
Bao la kwanza la Barcelona lilifungwa na Lionel Messi dakika ya 12, Andre Gomes akaiongezea timu yake bao pili, kabla ya Roberto Torres kuifungia Osasuna bao dakika ya 48.
Vao la tatu la Brca liliwekwa kambani ni Gomes dakika ya 57, dakika ya 61, Messi alifunga la nne, Francisco Alcacer aliiongezea timu yake bao la tano, kabla ya Javier Mascherano kufunga bao la sita dakika ya 67 na Alcacer kuiongezea bao la saba.
No comments