DC Kishapu awaagiza maofisa ugani kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akionesha
masuke ya zao la mtama wakati akikagua mojawapo ya mashamba ya wakulima wa Kata
ya Mwaweja wakati wa ziara yake.
Mkulima wa mtama, Mariam Nkinga (kulia) akiwaonesha Mkuu
wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu,
Shadrack Kangese mtama uliochanua katika shamba lake.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati)
akiangalia mtama katika shamba lililopo kata ya Mwaweja wakati wa ziara yake.
|
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati)
akiangalia mtama katika shamba lililopo kata ya Mwaweja wakati wa ziara yake.
|
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (wa pili
kulia) akibadilishana mawazo na mkulima, Sendama Luhende, Ofisa Kilimo, Sarai
Pura na mkulima Mariam Nkinga wakati wakikagua shamba.
|
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu akiendelea kukagua shamba la
mtama katika Kata ya Mwaweja.
|
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga akikagua shamba
darasa lililolimwa na Ofisa ugani Kata ya Uchunga, Aristidia Tasingwa.
Mwandishi Wetu, Kishapu
|
Ameagiza pia wananchi kulima mazao yanayostahimili
ukame hususan mtama na uwele badala ya kuwa na kasumba ya kung’ang’ania kilimo
cha mahindi ambacho katika sehemu kubwa ya wilaya hakifanyi vizuri.
Taraba alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake kwenye mashamba
ya mtama katika kata za Uchunga, Mwaweja na Ukenyenge kujionea na kufanya
tathmini ya kilimo wilayani humo.
Aliwataka maofisa hao kujiwekea utamaduni wa kutembelea
mashamba ili kuwafundisha namna ya matumizi ya mbegu bora kwani wengi wao
hupanda bila utaalamu.
Aliwataka kusimamia Sheria ndogo ya mwaka 2008 ya
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu inasisitiza kuwa kila kaya wilayani humo iweze
kulima ekari mbili za mazao yanayostahili ukame ambayo ni mtama.
Mkuu wa wilaya hiyo alisema kuwa hata hivyo wakulima
wengi wilayani humo wameweza kutekeleza sheria ndogo hiyo lakini wamepata
changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa maarifa ya matumizi ya aina sahihi za
mbegu.
“Ziara hii imetufundisha mambo mengi kwa mfano shambani
hapa tumeshuhudia wakulima hawa wametumia mbegu za aina tano tofauti katika
shamba moja sasa kama wangepata elimu wangetumia mbegu za aina moja zisizoshambuliwa
na ndege.
”Hivyo naagiza wataalamu wa kilimo wahamie mashambani
kufundisha wakulima na wawe na mashamba darasa yawe mfano wa kujifunzia wananchi
nao waige na kusonga mbele,” alisisitiza Taraba.
Aidha, alipiga marufuku wakulima kuuza wa mazao kwa
ajili ya matumizi mengine pasipo kujiwekea akiba na kuonya atakayefanya hivyo
atachuliwa hatua kali ikiwemo kupigwa faini.
Taraba ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama Wilaya alionya kuwa wapo baadhi ya wakulima wana tabia ya kufanya
biashara ya mtama kwa ajili ya kutengeneza pombe huku wao wakibaki bila ya chakula.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake mkulima wa mtama
katika Kata ya Mwaweja, Mariam Nkinga kwa niaba ya wenzake aliomba Serikali iwapelekee
mbegu fupi zinazokua kwa haraka.
Alisema wanapata changamoto ya mtama wao kuliwa na
ndege aina ya kwelea pamoja na wadudu ukiwa shambani kutokana na mbegu
wanazotumia kuchelewa kukomaa na hivyo kukaa muda mrefu shambani.
Nkinga alioimba wataalamu wawe wanapita mara kwa mara
kunyunyizia dawa mazalia ya wadudu na ndege waharibifu wa mazao ili wasiweze
kuzaliana na kufika mashambani.
Aliwashauri wananchi kulima zao la mtama kwa wingi na
kuacha kasumba ya kuchagua chakula na kulima mahindi ambayo matokeo yake
hawastawi yanakufa kutokana na ukame.
No comments