MALKIA WA TAARABU SHAKILA SAIDI AFARIKI DUNIA USIKU HUU JIJINI DAR
Habari
za kusikitisha zimetufikia muda huu kuwa malkia wa Tarabu nchini Bi.
Shakila Saidi amefariki dunia jioni ya leo muda mfupi baada ya kuanguka
na kukimbizwa hospitali ya karibu na nyumbani kwake Mbagala Charambe
jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika vilivyo karibu
na marehemu, Bi Shakila hakuwa anaumwa ila alianguka ghafla na
alipofikishwa hospitali akakata roho.
Taarifa kamili tutawaletea mara tu tutapozipata.
MOLA AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU - AMINA
No comments