
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
ujumbe wake wakishiriki katika Mkutano wa African Peer Review
Mechanism Forum (APRM)kwenye ukumbi wa hoteli ya Intercontinental jijini
Nairobi Agosti 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………
Mwandishi Wetu.
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa,
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, aliongoza ujumbe wa
Tanzania kwenye kikao cha 25 cha Wakuu wa Nchi wanaoshiriki kwenye
mchakato wa APRM. Pia walikuwepo Mheshimiwa Dkt Susan Kolimba, Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mheshimiwa
Dkt. Khalid S. Mohamed, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar. Kikao hicho kilifanyika mjini Nairobi, Kenya;
kuanzia tarehe 21-26 Agosti 2016 na kilihudhuriwa na jumla ya Wakuu wa
Nchi 22.
APRM ni Mpango wa Kujitathmini
Ki-Utawala Bora uliobuniwa na Wakuu wa Nchi za Kiafrika mwanzoni mwa
miaka ya 2000, ili kutatua changamoto za utawala bora zinazolikabili
bara la Afrika. Tanzania ni miongoni mwa nchi 35 zinazoshiriki kwenye
Mpango huu.
Kauli mbiu ya kikao hiki ni
“kuwa na APRM Imara itakayosaidia kuleta Mabadiliko katika Uongozi
barani Afrika” na hivyo kuendelea kuwa chombo kitakachosaidia katika
kufikiwa kwa malengo ya Umoja wa Afrika (Agenda 2063) na Malengo
Endelevu ya Maendeleo ya Umoja wa mataifa.
Kwa mara ya kwanza katika
historia ya kuanzishwa kwa Mpango huu, APRM ilipata muda wa siku
takriban sita za kuangazia kwa kina masuala mbalimbali ambayo ni pamoja
na Ripoti za Tathmini za nchi za Djibouti na Chad, Ripoti ya utekelezaji
wa Mpango kazi wa Nchi ya Msumbiji, Mpango Mkakati wa APRM 2016-2020,
Mpango Kazi na Bajeti kwa mwaka 2016/17, Masuala mbalimbali yanayohusu
utendaji wa Jopo la Watu Mashuhuri, Hati ya Kuinganisha APRM kama
Taasisi ndani ya Umoja wa nchi huru za Kiafrika, Taarifa ya Mkaguzi wa
Mahesabu ya APRM, Vianzio vya Fedha na Maeneo ya changamoto
yanayopendekezwa kuingizwa kwenye Hojaji Kuu ya APRM pamoja na
kuzingatiwa kwenye mbinu za tathmini y utawala bora kwa vipindi vijavyo.
Maeneo mtambuka katika Afrika
yaliyoonekana kuhitaji mikakati endelevu ya pamoja katika kuyatafutia
ufumbuzi ni pamoja na; Minyukano ya kimtazamo hasa juu ya itikadi, sekta
binafsi kutowezeshwa vya kutosha, miundo mbinu duni ikiwa nia pamoja na
nishati, barabara, reli, simu, mitandao ya mawasiliano n.k, dola
zisizokuwa imara, changamoto zihusuzo masoko, ukosefu wa viwanda pamoja
na usindikaji wa bidhaa usiyoridhisha, uhaba wa wataalam, maendeleo duni
katika sekta ya kilimo, maendeleo duni katika sekta ya huduma ikiwa ni
pamoja na benki, bima, utalii n.k, udhaifu kwenye mifumo ya kidemokrasia
na udhaifu wa uwajibikaji katika sekta ya umma. Baada ya mjadala wa
kina kuhusu maeneo yaliyotajwa hapo juu, ilikubalika kuwa, Hojaji Kuu ya
APRM pamoja na mbinu za tathmini zifanyiwe marekebisho ili kulenga
zaidi mambo hayo muhimu na hatimaye kuungezea mchakato wa APRM thamani
zaidi.
Tanzania inaendelea kutekeleza
Mpango kazi wa APRM kwa kushirikiana na Wizara, Idara na Wakala za
Serikali, pamoja na kuishirikisha Sekta Binafsi. Baada ya kushirikisha
wadau ili
No comments:
Post a Comment