Serikali yavishauri vyama, klabu, mashirikisho ya soka kuzingatia katiba zao
![]() |
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura |
Na Raymond Mushumbusi
Serikali imetoa mwito kwa vyama, klabu na nashirikisho
ya mpira wa miguu kuzingatia na kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa
katiba zao ili kupunguza migogoro inayoweza kujitokeza katika uendeshaji na
uendelezaji wa soka nchini.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura wakati akijibu swali la Mhe. Khatibu Saidi
Haji Mbunge wa Konde (CUF), kuhusu makosa yanayofanywa na klabu za soka
nchini kwa kupeleka mambo ya kisoka katika mahakama ambapo ni kinyume cha sheria za FIFA.
Annastazia Wambura amesema ni kweli kuwa
Sheria za FIFA zinakataa mambo yanayohusiana na soka kupekekwa mahakamani hivyo
hatua hiyo ya Vyama na Klabu kuzingatia Sheria na taratibu inalenga kuwezesha
masuala ya soka kuendeshwa kwa kuzingatia taratibu na miongozo iliyowekwa na
Mamlaka za Michezo huo kwa ngazi mbalimbali.
Aidha amesema hatua hiyo imewezesha mchezo wa
soka kuchezwa na kupata matokeo kwa wakati
na hivyo kuepusha mazuio ya mahakama ambayo yanaweza kusababisha usumbufu usio
wa lazima kwa washiriki wengine hata kupelekea kufungiwa kwa Shirikisho la Soka
Tanzania(TFF).
Maendeleo
ya michezo hapa nchini yanaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Michezo
ya mwaka 1967, kama ilivyorekebishwa kwa mujibu wa Sheria Na 6 ya mwaka 1971
lakini bado Sheria hii inakinzana na
Sheria za FIFA ila serikali inafanya mapitio ya Sheria hiyo ili iendane na
wakati kwa lengo la kuboresha na kuendeleza michezo nchini.
No comments