BENCHI la ufundi la Simba SC jana limeukagua Uwanja wa
Estadio Libolo itakakochezwa mechi ya kesho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya
Wekundu na Libolo na kubaini siri nzito.
Vipimo vya Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig, vilibaini
kwamba uwanja huo una upungufu wa takribani mita sita kwa urefu na upana
kulinganisha na viwanja vingi vya soka.
Kwa mujibu wa Liewig, uwanja huo umepunguzwa ukubwa ili
kusaidia timu ya Libolo ambayo inafahamika sana kwa kufunga mabao mengi ya
mipira iliyokufa (adhabu, kurusha n.k).
“Kutokana na hali hii, maana yake ni kwamba kila itakapokuja
kona, itakuwa hatari kwa sababu kuna umbali mdogo kutoka kwenye kona hadi goli.
Itakuwa hatari hivyohivyo kwenye mipira ya kurusha na ya adhabu. Ni muhimu
tumeliona hili mapema,” alisema.
Alisema atawaeleza wachezaji wake kujiepusha kutoa kona au
mipira ya kurusha bila ya sababu kwa vile inaonekana hiyo ndiyo silaha kubwa ya
wapinzani hao wa Simba.
“Kama unakumbuka, hata goli lao la Dar lilitokana na mpira
wa kurusha halafu ikapigwa krosi. Ndiyo maana nafikiri wameleta mechi hii huku
badala ya Luanda ili watumie faida hii vizuri,” alisema.
Nchini England, Uwanja wa Britannia unaotumiwa na timu ya
Stoke City inayocheza Ligi Kuu ya nchi hiyo unafahamika pia kwa kuwa mdogo
kwenye eneo la kuchezea kuliko viwanja vingi vya nchi hiyo.
Hata hivyo, inaelezwa kwamba lengo kuu la kuuweka uwanja huo
katika eneo hilo ni kutumia nguvu ya mipira ya kurusha na adhabu nyingine
ambayo ndiyo silaha kubwa ya Stoke. Miaka miwili iliyopita, robĂ´ ya magoli
yaliyokuwa yakifungwa na timu hiyo yalitokana na mipira ya kurusha ya Rory
Delap.
No comments:
Post a Comment