MBWANA Samatta, mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Lubumbashi, DR Congo, alitumia vizuri pasi iliyotoka kwa Frank Domayo na kuukwamisha mpira wavuni dakika ya 90.
Bao hilo
lilitokana na makosa ya kipa wa Cameroon,
Komguep aliyeruka juu kutaka kuokoa mpira huo, lakini ukatua miguuni mwa
Samatta na kuusindikiza wavuni.
Katika mchezo, Taifa Stars
walianza kwa kasi na kulishambulia lango la Cameroon, dakika ya nne
walifanikiwa kulifikia lango la wapinzani wao, lakini walishindwa kujipatia bao
la haraka.
Ndani ya dakika saba ya
kipindi cha kwanza, mshambuliaji wa kimataifa wa Taifa Stars, Mbwana Samatta,
alichezewa vibaya mara tatu.
Wakicheza kwa kuonana vizuri,
Frank Domayo na Abubakari ‘Sure Boy’, waliweza kuwasumbua viungo wa Cameroon dakika
ya 12, huku kipa Juma Kaseja akiwa mapumziko.
Cameroon walipata nafasi nzuri ya bao, kufuatia mpira wa kona,
lakini beki kisiki wa Stars, Kelvin Yondan aliondoa hatari hiyo langoni kwao.
Dakika ya 14, Kaseja alipata
maumivu kidogo baada ya kuangukiwa na
mshambuliaji wa Cameroon,
Tchami Herve, lakini baada ya kutibiwa aliendelea kukaa langoni.
Cameroon walifanya shambulizi la nguvu dakika ya 24, lakini
shuti kali la Tchami lilitoka nje kidogo ya lango la Stars, huku Kaseja akiwa
amesimama bila ya kujaribu kuufuata mpira.
Mashambulizi ya Stars
yalifanikiwa kuwachanga mabeki wa Cameroon
na kuzaa penalti baada ya beki mmoja wa timu hiyo kuunawa mpira ndani ya eneo
la hatari na mwamuzi Munyemana Hundu kutoka Rwanda kupuliza filimbi ya adhabu
hiyo.
Beki wa Stars, Erasto Nyoni,
alikosa penalti hiyo baada ya kipa wa Cameroon, Effala Komguep, kuudaka
mpira huo.
Stars walikianza kipindi cha
pili kwa kuliandama lango la wapinzani wao, ambapo dakika ya 49, lakini krosi
ya Nyoni ilitoka nje ya lango.
Stars wakicheza soka safi na kuwafanya Cameroon, washindwe kumfikia kipa
Juma Kaseja, kwa muda wa dakika 29, wakati dakika ya 78, Thomas Ulimwengu alishindwa
kuunganisha vizuri kwa kichwa mpira wa krosi uliopigwa na Mbwana Samatta.
Kwa ushindi huo, Stars
itakuwa inajitengenezea nafasi kubwa ya kuombwa mechi za kirafiki na nchi
nyingine zilizo bora katika soka barani Afrika.
Mwanzoni mwa mwaka huu, Stars
ilifanikiwa kuwachapa mabingwa wa Mataifa ya Afrika mwaka jana, Zambia ‘Chipolopolo’,
bao 1-0, bao lililofungwa na Mrisho Ngassa.
Matokeo hayo ndiyo yaliyowavutia
Cameroon,
mpaka wakaomba kucheza mechi ya kirafiki na Stars, hivyo baada ya kipigo cha
leo, itakuwa imepanua wigo zaidi wa mataifa mengine kuomba mechi ya kirafiki.
Stars: Juma Kaseja, Erasto
Nyoni, Shomari Kapombe, Kelvin Yondan, Aggrey Morris, Salum Abubakari ‘Sure
Boy’, Mrisho Ngassa, Frank Domayo, Mbwana Samatta, Mwinyi Kazimoto/Thomas
Ulimwengu, Amri Kiemba.
Cameroon: Effala Komguep,
Assout Ekotto, Aminou Bouba, Ngoula Patrick, Nyom Allan, Pierre Wome, Kiunge
Mpondo, Benino Henry, Tchami Herve/Elounu, Olinga Fabrice, Aboubakar Vincent.
No comments:
Post a Comment